Marioo Azungumzia Tuhuma za Wasanii wa Bongo Kuiga Wimbo Wake ‘Beer Tamu’

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Marioo amefunguka kuhusu tuhuma zinazodai kuwa baadhi ya wasanii wa bongo wameiga wimbo wake wa ‘Beer Tamu’.

Kwa siku za hivi karibuni, wasanii wengi wa bongo wamekuwa wakiachia nyimbo za burudani ambazo zinasifu vileo. Nyimbo hizi zimetengenezwa na lengo kuu la kuwaburusisha mashabiki haswaa wale walioko sehemu za burudani.

Soma Pia: Marioo Aeleza Sababu ya Albamu Yake Kuchelewa

Mtindo wa wasanii kusifu pombe na burudani ulitokea muda mfupi baada ya Marioo kutoa ngoma yake ya ‘Beer Tamu’.

Jambo hili liliibua mjadala mtandaoni kuwa wengi wa wasanii hao walikuwa wameiga wimbo wa Marioo. Kupitia mahojiano ya hivi karibuni na Wasafi TV, Marioo alitoa kauli yake kuhusu tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa msanii huyo, haiwezekani kuwa wasanii hao waliiga wimbo wake kwa asilimia mia. Aliwatetea kwa kusema kuwa kuna muda ambapo wasanii hujikuta na fikra zinazofanana ikija katika kutunga nyimbo.

Soma Pia: Marioo Ajibu Madai ya Kutumia Ushirikina ili Kufanikiwa Kimuziki

"Unajua inawezekana kati ya ngoma ulizotaja hizo, inawezekana chache sana ndizo zimefanywa kwa sababu mimi nimefanya. Lakini kuna muda ambapo wasanii huwaga tunafikiria kitu moja. Wewe uko chumba hiki unafanya kazi, mwenzako yuko Mbagala lakini naye akatengeneza idea kama hiyo. Lakini mimi nawezasema labda inawezekana mimi nimetoa tu kushinda wao, lakini sidhani kuwa inawezekana a hundred percent kuwa mimi nimetoa Beer Tamu ime hit nao wametoa," Marioo alieleza.

Leave your comment