Marioo Ajibu Madai ya Kutumia Ushirikina ili Kufanikiwa Kimuziki

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Marioo amefunguka na kujibu tuhuma zinazoashiria kuwa yeye hutumia nguvu za uganga ili afanikiwe kimuziki.

Marioo wakati alikuwa anahojiwa na Wasafi TV, aliarifiwa kuwa wapo baadhi ya mashabiki ambao wanaamini kuwa nyota yake katika tasnia ya muziki inang'aa kwa sababu ya nguvu za giza.

Soma Pai: Marioo Adhibitisha Ujio wa Kolabo Zake na Alikiba, Diamond Platnumz

Marioo alikana madai hayo vikali na kusisitiza kuwa mafanikio yake yanatokana na ubora wa muziki wake pamoja na bidii.

Aidha, Marioo alieleza kuwa yeye kibinafsi kama msanii hujitahidi sana ili aweze kuachia kazi yenye ubora wa hali ya juu. Aliongezea kuwa anawekeza muda mwingi pamoja na pesa nyingi katika miradi yake ya muziki.

Soma Pia: Marioo Adai Yeye Ndiye Muanzilishi wa Swahili Amapiano

Ni bidii hii ndio mwisho wa siku hufanya muziki wake kuvuma na kupata mafanikio mengi na kuwafanya baadhi ya mashabiki kuamini kuwa huenda anatumia mbinu zingine zisizofaa.

Marioo pia aliongeza kuwa yeye hajawahi enda kwa mganga maishani mwake. Kwa siku za hivi karibuni, Marioo amekuwa akipata mafanikio makubwa sana kwenye muziki na kwa sasa nyota yake inang'aa zaidi kuliko hapo awali.

Nyimbo anazotoa Marioo zimepata mamilioni ya watazamaji kwenye mitandao ya kusikiliza na kutazama muziki. Kwa mfano, wimbo wake mpya Marioo uliopewa jina la ‘Beer Tamu’ umetazamwa takriban mara milioni moja nukta nne ndani ya siku kumi na mbili ya uchapisho wake kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment