Marioo Aeleza Sababu ya Albamu Yake Kuchelewa

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu Marioo kutoka bongo amezungumzia sababu kuu ambayo imefanya albamu yake kuchelewa kutoka.

Hapo awali Marioo alitangaza kuwa mwaka huu ataachia albamu yake ya kwanza. Ikiwa imesalia takriban mwezi mmoja na nusu, hakuna dalili za yeye kutoa albamu na hajazungumzia suala hilo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video ya Wimbo wake wa Amapiano 'Beer Tamu'

Kupitia mahojiano na Wasafi TV, Marioo alidhibitisha kuwa albamu hiyo bado ipo njiani ila amelazamika kuichelewesha kwa sababu kadhaa.

Marioo alieleza kuwa albamu inahitaji kazi nyingi mno na hivyo basi katika utengenezaji wake, alikumbana na masuala yalioelekeza kucheleweshwa kwake. Marioo, hata hivyo, aliongezea kwa haraka kuwa albamu hiyo itatoka mwishoni mwa mwaka huu au mapema mwaka ujao.

Soma Pia: Marioo Atangaza Ujio wa Ziara Yake ya Muziki Nchini Tanzania

Msanii huyo alisema albamu ni ya maana sana kwa taaluma yake ya muziki haswaa kwa wakati huu ambapo yeye anavuma mtandaoni. Alieleza kuwa mashabiki kwa sasa wangependa kujua iwapo ako na uwezo wa kuvuma kwa kiasi sawia kama atatoa ngoma zaidi ya kumi na tano, au yeye anavuma kwa ngoma moja tu.

Marioo pia alieleza kuwa kutokana na sababu ya kuwa hii ni albamu yake ya kwanza, ameamua kuwekeza muda mwingi katika utengenezaji wake ili atoe albamu ambayo itakuwa na ngoma bora toka mwanzo hadi mwisho.

Kwa hivyo, aliwasihi mashabiki wake wawe wenye subira kidogo kwani albamu bado ipo jikoni inaiva. Baadhi ya wasanii wengine wakubwa ambao wameachia albamu zao mwaka huu ni pamoja na Harmonize na Alikiba huku Diamond Platnumz akisubiriwa kuachia yake hivi karibuni.

 

Leave your comment