Hussein Machozi Asifu Albamu ya Harmonize

[Picha: Yinga Media]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mmoja wa wanamuziki wakongwe kutoka bongo Hussein Machozi ameisifu albamu mpya ya ‘High School’ kutoka kwake msanii Harmonize.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Hussein Machozi alisema kuwa albamu ya Harmonize ‘High School’ ina ubora wa hali ya juu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia ‘High School’ Album

Aliendelea kwa kusema kuwa kwake yeye binafsi albamu hiyo ndio bora kwa mwaka huu. Alimpongeza Harmonize kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kutengeza albamu hiyo.

Hussein Machozi aliwashauri watumiaji wa mitandao ya kijamii wakachukue muda wao na kuisikiliza albamu hiyo ili waburudishwe pia. Hussein vile vile alichapisha picha iliyomwonyesha akiwasiliana na Harmonize kupita mtandao wa kijamii.

Soma Pia: Harmonize Aeleza Tofauti Iliokuwepo Katika Utengenezaji wa Albamu ya Afro East na High School

Msanii huyo, hata hivyo, hakufichua kile ambacho walikuwa wakizungumzia.

"Mipango mikubwa #HIGHSCHOOL ni noma sana kusema ukweli..kwangu mimi hii ni the best album ever @harmonize_tz me sisemi sana wacha watu waenjoy," chapisho la Hussein Machozi mtandaoni ulisomeka.

Kauli ya Hussein Machozi kuhusu albamu ya Harmonize inabeba uzito mwingi haswaa ikizingatiwa kuwa amekuwepo kwenye tasnia ya muziki wa bongo kwa muda mrefu sana.

Hussein ni mmoja wa wasanii ambao walivuma katika enzi za bongo ya kale.

Albamu ya ‘High School’ ambayo iko na jumla ya nyimbo ishirini kutoka kwa Harmonize imepokelewa vyema na mashabiki.

Albamu hiyo tayari ishasikilizwa zaidi ya mara milioni moja katika jukwaa tofauti ya kusikiliza miziki mitandaoni. Harmonize kwa sasa amebakisha kuachia video za nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo.

Leave your comment