Harmonize Aeleza Tofauti Iliokuwepo Katika Utengenezaji wa Albamu ya Afro East na High School

[Picha: NME]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Imesalia masaa machache kabla ya msanii nyota Harmonize kuachia albamu yake iliyosubiriwa sana ya 'High School'.

Hii itakua albamu ya pili kutoka kwa msanii huyo, huku albamu yake ya kwanza ikiwa 'Afro East' aliyoiachia mapema mwaka jana.

Kabla ya 'High School' kutoka, Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram amewasimulia mashabiki wake utofauti aliyoupitia katika safari ya utengenezaji wa albamu hizo mbili.

Soma Pia: Harmonize Adokeza Ujio wa Ngoma Mpya ya Singeli ya Kiingereza

Ikumbukwe kuwa Harmonize aliachia albamu ya 'Afro East' baada ya kuondoka lebo ya WCB ambayo ilimtambulisha kwenye tasnia ya muziki.

Kwa mujibu wa Harmonize, alikuwa mwingi wa wasi wasi wakati akitengeneza albamu ya ‘Afro East'. Hii huenda ikatokana na sababu kuwa 'Afro East' ilikuwa albamu yake ya kwanza.

Vile vile kwa wakati huo, macho yote yalikuwa kwake haswaa baada ya kutoka WCB na wengi walikuwa wamesubiri kuona iwapo angefanikiwa au angedidimia kimuziki kama vile wasanii wengine walioondoka lebo hiyo.

Soma Pia: Dancer wa Diamond Angel Nyigu Azungumzia Uwezekano Wake Kufanya Kazi na Alikiba, Konde Gang

Kwa upande mwingine hali ilikuwa tofauti wakati wa utengenezaji wa albamu ya 'High School'. Harmonize alisema kuwa kwa wakati huu alikuwa mtulivu wa mawazo.

“Trust me when I was making #AfroEast I was so worried itakuwaje #Highschool Smocking everyday. See You on November (5) Happy New month my People,'' chapisho la Harmonize mtandaoni lilisomeka.

Albamu ya ‘High School’ ina jumla ya ngoma ishirini.

Leave your comment