Babu Tale Aomba Mkubwa Fella Ajengewe Sanamu Kwa Mchango Wake Katika Kukuza Vipaji Vya Wasanii

[Picha: Mkubwa Fellatmk Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Babu Tale Aomba Mkubwa Fella Ajengewe Sanamu Kwa Mchango Wake Katika Kukuza Vipaji Vya Wasanii - Sikulu

Babu Tale, meneja wa mwanamuziki nyota Diamond Platnumz, ameomba kuwa mlezi wa vipaji vya muziki Mkubwa Fella ajengewe sanamu mjini Temeke kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki.

 Mkubwa Fella amehusika pakubwa katika kuwatoa baadhi ya wanamuziki ambao kwa sasa wanaheshimaka Afrika Mashariki. Miongoni mwa wasanii waliopitia mikononi mwa Mkubwa Fella ni pamoja na bendi ya kale iliyovunjika ya Yamoto Band.

Soma pia: Nyimbo Tano zinazovuma Bongo Wiki hii

Kwa mujibu wa Babu Tale, kando na kujengewa sanamu kama ishara ya heshima kwa kazi yake kwenye tasnia ya muziki, Mkubwa Fella anafaa kuekewa tamasha na wasanii wa Yamoto Band. Babu Tale alieleza kuwa Mkubwa Fella alihusika pakubwa katika kulea vipaji vya waliokuwa wanachama wa bendi ya Yamoto. Wanachama hao walikuwa; Enock Bella, Beka Flavour, Aslay na Mbosso.

"Mkubwa Fela anastahili sanamu ya heshima. Usiku wa jana sijalala kabisa, kwani nilizongwa na kumbukumbu ya safari ya Muziki na maisha. Mbali ya kuwakumbuka watu wengi, Kichwani mwangu ilikuja picha ya darasa lenye Watoto Wanne wenye Masauti yanayogonganisha mashairi yasiyochosha," Babu Tale alisema.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video ya Ngoma Yake 'Inatosha'

"Ni kweli nilikuwa nikiliwaza darasa lenye historia kubwa nalo ni "Yamoto Band". Ni miaka mingi imepita toka kundi hili lililowahi kuwa na mvuto mkubwa livunjike. Na leo sijawaza juu ya kwanini limevunjika!?..Bali nimewaza na kutafakari Uthubutu, Malengo, Kujitoa na Uwekezaji uliofanywa na @mkubwafellatmk Kwa hakika Natamani kuona Kundi hili lilowahi kuundwa na @mbosso_ @enockbellaofficial @bekaflavour na @aslayisihaka wanaandaa Tamasha la kutambua, kushukuru na kumpongeza Mkubwa Fella," aliongezea.

Leave your comment