Ray C Asikitishwa na Utengano Katika Tasnia ya Muziki Tanzania

[Picha: All Africa]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii nyota Ray C ameelezea kusikitishwa na utengano uliopo kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wake wa Instagram, Ray C alieleza kwa kina jinsi utengano huu umeathiri vibaya muziki wa bongo. Msanii huyo ambaye ni mmoja wa wanamuziki wakongwe sana wa muziki wa bongo alisistiza kuwa utengano ni udhaifu.

Soma Pia: Ibraah Apendezwa na ‘High School’ Album ya Harmonize, Aitaja Albamu Bora Afrika

Kwa mujibu wa Ray C, inawezakana kuleta umoja baina ya wasanii wa Tanzania. Alikiri kuwa yeye kibinafsi anatamani sana ifike siku ambayo wasanii wa bongo watapendana na kuungana mkono.

Malkia huyo wa muziki wa bongo aliashiria kuwa huenda uhasama baina ya wasanii umeleta visa vya wengine wao kuzomewa wakati wako jukwaani wakiburudisha. Aliendelea kwa kutoa kauli yake kuhusu ziara ya wasanii wa bongo Diamond Platnumz na Harmonize kule Marekani.

Soma Pia: Rayvanny Adai Chuki Inaathiri Vibaya Ukuaji wa Tasnia ya Muziki Tanzania

Kulingana na Ray C, haijalishi nani amejaza katika onyesho na nani hajajaza. Cha muhimu ni kuwa wasanii hao wanatoka taifa moja na hivyo wanafaa kuungwa mkono kwa pamoja bila ya ubaguzi.

"Umoja ni Nguvu. Utengano ni Udhaifu..Natamani ije siku nione haya kwa wasanii wetu wapendwa. Itapendeza sana.Itavutia mno.Inawezekana kabisa sijui tatizo nini hasa. Hivi kweli ndio hali imefikia hivi? ya kutumiana watu kwenye mashow na kuzomeana jamani?Nani kajaza nani hajajaza? Kweli? wote kutoka nchi moja?????This is too much aisee.Haipendezi hata kidogo Mashindano kwenye biashara yoyote yapo ila sio kwa style hii...Sio sawa kabisa ...Why? To be honest Am sad," ujumbe wa Ray C mtandaoni ulisomeka.

Leave your comment

Top stories

More News