Rayvanny Adai Chuki Inaathiri Vibaya Ukuaji wa Tasnia ya Muziki Tanzania

[Picha: Nairobi Wire]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota Rayvanny amedai kuwa chuki ni miongoni mwa vigezo ambavyo vinaathiri vibaya ukuaji wa tasnia ya muziki nchini Tanzania.

Nyota huyo kupitia ukurasa wake wa kijamii alidai kuwa muziki wa bongo upo kwenye njia sahihi na anapenda unakoelekea.

Soma Pia: Harmonize Afichua Idadi ya Nyimbo na Wasanii Walioshirikishwa Kwenye ‘High School’ Album

Aliongeza kwa haraka kuwa kikwazo kikubwa kitakacho zuia maendeleo kwenye muziki wa Tanzania ni chuki na uhasama miongoni mwa wanamuziki.

Kwa mujibu wa Rayvanny, wasanii wanafaa kufurahia mafanikio ya mmoja wao na wala si kuumia wanapomwona mwenzao akipiga hatua kwenye muziki.

Soma Pia: Wasifu wa Mac Voice,maisha yake ya mapema, kazi yake ya sanaa...

Bosi huyo wa lebo ya Next Level Music alitamatisha ujumbe wake kwa kusema kuwa yeye kibinafsi anamuunga mkono msanii yeyote ambaye anafanya muziki mzuri.

"Muziki wetu unapoenda sio pabaya na utafika mbali tukiacha chuki na kuumia unapoona mwenzako anafanya vizuri ... Wenzetu mmoja wao akifanya vizuri wote wanamsapoti basi nasisi tufanye kama wenzetu ili tufike mbali. Nasapoti kila anaefanya vizuri sababu mmoja akifanikiwa imefanikiwa industry yetu lets go global," kauli ya Rayvanny kwenye mtandao ilisomeka.

Kauli hii kutoka kwa Chui inatokea wakati ambapo kumeibuka mjadala kuwa huenda muziki wa bongo unadidimia na ukaisha kwa siku za usoni.

Mjadala huu ulitokana na wasanii wengi wa bongo kuenda na upepo wamuziki wa mitindo nyingine zikiwemo Swahili Amapiano. Muziki wa bongo ni mmoja katika ya mitindo ya muziki wa kale Afrika Mashariki na ni kitambulisho cha Tanzania kwenye tasnia ya muziki.

Leave your comment