Rayvanny Adokeza Ujio wa Ngoma Yake Mpya

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota kutokea lebo ya Next Level Music Rayvanny amedokeza kwa mashabiki zake kuhusu wimbo mpya ambao anatarajiwa kuutoa hivi karibuni.

Rayvanny ambaye amekaa takriban mwezi mmoja bila kutoa ngoma yoyote ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Soma Pia: Rayvanny Adai Chuki Inaathiri Vibaya Ukuaji wa Tasnia ya Muziki Tanzania

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliweka kipande kidogo cha ngoma hiyo na kuisindikiza na ujumbe ‘Global Way New Chui 29/01/2021’.

Ujumbe huo una maana kuwa Rayvanny anatarajia kuachia ngoma hiyo siku ya tarehe 29 November, tarehe ambayo pia mwanamuziki Alikiba ametangaza kuachia video ya mojawapo ya ngoma kutoka kwenye albamu yake ya ‘Only One King’ aliyoiachia mwezi huu.

Soma Pia: Rayvanny Ashukuru Mashabiki Kwa Mapokezi Mazuri Waliompa Mac Voice

Taarifa hii imepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa muziki kwani mara ya mwisho Rayvanny aliachia ngoma ya ‘Wanaweweseka’, na tangu hapo, hajatoa ngoma yoyote bali amekuwa akimpa nafasi msanii wake Mac Voice ambaye wameshirikiana kwenye ngoma mbili ambazo ni ‘Tamu’ pamoja na ‘Pombe’.

Rayvanny kwa muda sasa amekuwa akidokeza kupitia mitandao ya kijamii na mahojiano na vyombo vya habari mbalimbali kuhusu ujio wa EP yake ya pili tangu aanze muziki ya kuitwa ‘Flowers II’.

‘Flowers II’ ni muendelezo wa EP yake ya ‘Flowers’ ambayo aliiweka sokoni mwanzoni mwa mwaka 2020.

Leave your comment