Alikiba Azungumzia Alivyolazimika Kubadilisha Mtindo wa Kutoa Ngoma

[Picha: Wikipedia]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu Alikiba kwa muda mrefu amejulikana kama msanii anayetoa ngoma moja na kisha kukimywa kiasi kabla ya kuachia ngoma nyingine.

Mwaka huu hata hivyo, Alikiba alibadilisha mtindo wake na kuanza kutoa nyimbo mfululizo, jambo ambalo limemfanya kuwa gumzo sana miongoni mwa wadau tofauti kwenye tasnia ya muziki haswaa mashabiki.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu ya Kuita Albamu Yake ‘Only One King’

Japo mtindo huu mpya ulitokana na ujio wa albamu yake ya 'Only One King', Alikiba ameeleza kwa kina baadhi ya sababu nyingine ambazo zilimfanya kubadili mtindo wake.

Alikiba alieleza kuwa hapo awali alikuwa akizingatia kipato ambacho anapata kwenye wimbo kabla ya kutoa ngoma nyingine. Alisema kuwa alisubiri apate hela alizoekeza kwenye ngoma moja ndipo atoe tena nyingine, jambo hili lilimfanya kwa wakati mwingine kukimya kwa muda mrefu sana.

Soma Pia: Alikiba Azungumzia Killy na Cheed Kuondoka Kings Music

Kulingana na Alikiba, mashabiki wake hawakuelewa kuwa huu ulikua mtindo wake na hivyo basi wakaanza kulalamika. Mwaka huu, hata hivyo, alilazimika kubadilisha mfumo wake kwa sababu ya malalamiko kutoka kwa mashabiki. Aliongeza kuwa kwa sasa anataka kuwafurahisha na pia kuwaburudisha mashabiki wake.

Alikiba, ambaye amedaiwa kuwa mfalme wa muziki wa bongo, alifafanua kuwa mashabiki ndio msingi wa kila msanii na hivyo basi inafika wakati ambapo msanii anafaa kuzingatia mashabiki wake zaidi.

Leave your comment