Alikiba Azungumzia Killy na Cheed Kuondoka Kings Music

[Picha: Mullastar]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

 Mwanamuziki tajika kiwanda cha Bongo Fleva Alikiba hivi karibuni amezungumza kwa uwazi kuhusu wasanii Cheed na Killy kuondoka kwenye lebo yake ya Kings Music mwishoni mwa mwaka jana.

Akiwa anajibu swali aliloulizwa na Lil Ommy kuhusu wasanii hao kuondoka kwenye lebo yake, Alikiba aliweka bayana kuwa hakuwa na mkataba wa kimaandishi na wasanii hao, kwa hivyo, wao kuondoka aliona ni jambo la kawaida tu.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu ya Kuita Albamu Yake ‘Only One King’

Alikiba alisema nia yake ilikuwa ni kukuza vipaji vya wasanii hao ili wawe wakubwa kwenye tasnia ya Bongo na barani Afrika.

"Lengo ni mkataba tu kwa sababu sikuwa na mkataba na msanii yeyote. Nionekane nimefanya kitu na mimi nina mchango wangu kwenye Bongo Fleva amefanikiwa anafanya kazi zake hiyo kwangu inatosha," alizungumza Alikiba.

Soma Pia: Albamu 3 Zitakazosisimua Tasnia ya Muziki Tanzania

Alikiba pia alitumia fursa hiyo kuweka bayana kuwa yeye hana mgogoro wowote na msanii Ommy Dimpoz, kama ambavyo watu wengi hufikiri. Aliongeza kuwa kwa sasa kila mtu anafanya vitu vyake kutokana na kuwa na majukumu tofauti.

"Kwanza Ommy Dimpoz nimefanya nae ngoma nyingi sana lakini vile vile Ommy Dimpoz sasa hivi yuko tight kidogo ana kazi zake sasa hivi anafanya. Anafanya matangazo. Hakuna kitu kusema labda tumegombana, sio ishu za management wala nini," alitanabaisha Ali Kiba.

Leave your comment