Nandy Atoa Ratiba ya Ziara Yake ya Mwishoni mwa Mwaka

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Idadi kubwa ya wasanii wa bongo kwa sasa wamo mbioni kufanikisha ziara zao za muziki katika sehemu tofauti duniani.

Baadhi ya wanamuziki tajika ambao wanaendelea na ziara yao ya muziki ni Harmonize na Diamond Platnumz ambao kwa sasa wako Marekani.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Inatosha’, Nandy ‘Kunjani’ na Ngoma Zingine Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Wasanii wengine kama vile Marioo wametangaza kuanza ziara yao nyumbani Tanzania. Malkia wa muziki wa bongo Nandy pia ameachia ratiba ya ziara yake ambayo itakua ndani na nje ya bara la Afrika.

Ziara hiyo ambayo ilianza tarehe 23 mwezi Oktoba itaendelea hadi tarehe 31 mwezi Disemba. Ziara ya Nandy itahusisha mataifa mengi tofauti na pia miji kadhaa ndani ya Tanzania.

Soma Pia: Wasifu wa Mac Voice,maisha yake ya mapema, kazi yake ya sanaa...

Sehemu mingi iliyopo kweye ziara ya Nandy zipo Afrika isipokuwa Dubai ambako Nandy atatua kutoka tarehe 26 hadi tarehe 28 mwezi Novemba.

Nandy atazuru mataifa ya Afrika Mashariki, Afrika Magharibi na vile vile Afrika kusini. Baadhi ya mataifa yaliyo orodheshwa kwenye ziara ya Nandy ni; Afrika Kusini, Kenya, Tanzania na Nigeria.

Nandy amesifiwa sana kutokana na mafaniko yake ikija kwenye ziara ya muziki. Amejulikana na tamasha yake ya Nandy Festival ambayo huwa anatumia kila mwaka kuzuru sehemu tofauti za taifa la Tanzania.

Nandy huwaleta wasanii kutoka ndani na nje ya Tanzania kuwaburudisha mashabiki. Ziara ya muziki ni muhimu kwa msanii kwani ni mojawapo ya njia kuu ambayo msanii hupokea kipato chake.

Leave your comment