Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Inatosha’, Nandy ‘Kunjani’ na Ngoma Zingine Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Soko la muziki nchini Tanzania limeendelea kupokea bidhaa tofauti tofauti kutoka kwa wasanii ambao wameachia ngoma ambazo zimeburudisha mashabiki. Hizi hapa ni ngoma tano kali mpya ambazo zimeachiwa na kufanya vizuri sana Tanzania wiki hii:

Soma Pia: Mac Voice Asimulia Alivyohangaika kufanya Muziki Hadi Karibu Ajitoe Maisha

Inatosha - Lavalava

Baada ya ukimya wa takriban miezi mine, hatimaye Lavalava wiki hii aliachia ngoma yake ya kuitwa ‘Inatosha’. Kwenye ngoma hii, anatumia mtindo wa nyimbo za zamani kufikisha ujumbe wake. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara laki mbili hamsini na nne kwenye mtandao wa YoutTube.

https://www.youtube.com/watch?v=5iD2KmJkhb0

Kunjani - Nandy ft Sho Madjozi

Kama unapenda muziki wa Amapiano basi bila shaka utapenda ngoma hii mpya ya Nandy ya kuitwa ‘Kunjani’ ambayo ameshirikiana na Sho Madjozi kutokea Afrika Kusini. ‘Kunjani’ ni neno la kizulu ambalo hutumika pale mtu anapotaka kukujulia halI. Bila shaka hii ni ngoma ambayo itakufanya ucheze na kufurahi kutokana na mdundo mzuri utakaokuchangamsha

https://www.youtube.com/watch?v=33QNth6LAhM

Kawaida - Lulu Diva

Kwenye ngoma hii ambayo imeandikwa na Whozu, Lulu Diva amezungumzia vitu mbalimbali ambavyo watu wanaona ni vya ajabu, ila yeye anaona ni vitu vya kawaida tu. Kama unatafuta ngoma ambayo itakufanya ucheze na kufurahi basi hii ni kwa ajili yako.

https://www.youtube.com/watch?v=wvt6432F11E

Shindulia Chini - Dogo Janja ft Mimi Mars

Ngoma hii imetayarishwa na Genius Jini na inafaa hasa kwenye maeneo ya club na sehemu za kujirusha kutokana na mdundo kuwa wa kuchangamka.

https://www.youtube.com/watch?v=OeFmI1zD2RI

Nyumba - Dully Sykes

Mwanamuziki Dully Sykes ameamua kusema ya moyoni kwa jinsi gani ananyanyasika kwenye jamii kutokana na kutokuwa na nyumba. Malalamiko hayo ameyawasilisha kupitia ngoma yake mpya ya kuitwa ‘Nyumba’. ‘Nyumba’ ni ngoma iliyotayarishwa na Banx ambaye ameshirikiana na Mr Touch.

https://www.youtube.com/watch?v=tYMxw6esPRQ

Leave your comment