Yogo Beats Azungumzia Madai Kuwa Alikiba Amemkataza Kufanya Kazi na Wasanii wa WCB

[Picha: Wikimedia]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji wa muziki wa kuheshimika kutoka Tanzania Producer Yogo Beats amekana madai kuwa Alikiba amemkataza kufanya kazi na lebo pinzani kama vile WCB.

Tuhuma hizi zimeibuka mtandaoni kutokana na Alikiba kufanya kazi na Producer Yogo pekee yake kwa muda mrefu. Yogo kwa upande mwingine licha ya kufanya kazi na baadhi ya wasanii wa bongo, hajawahi husika katika utengenezaji wa kazi za wasanii wa lebo ya WCB.

Soma Pia: Producer Yogo Beats Asikitishwa Kuona Albamu ya Alikiba Ikiuzwa Mtaani

Alikiba ni mpinzani mkuu wa mwanamuziki nyota Diamond Platnumz ambaye anamiliki lebo ya WCB, hivyo basi tetesi zimeibuka kuwa huenda hii ndio sababu kuu ya Producer Yogo kutokuwa na ukaribu na WCB.

Yogo Beats akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni amesisitiza kuwa yeye ni producer huru na hajakatazwa kufanya kazi na msanii yeyote.

Alieleza kuwa yeye ni mfanyibiashara na hivyo basi atafanya kazi na msanii yeyote ule ata kama ni Diamond Platnumz, bora makubaliano yampendeze. Yogo alisema kuwa tatizo ambalo Alikiba hukua nalo na watayarishaji wa muziki ni usiri wa kazi.

Soma Pia: Yogo Beats Ajibu Madai ya Kupuuza Wasanii Wengine Alipokuwa Akiandaa Albamu ya Alikiba

"Mimi ni producer huru ambaye anaruhusiwa kufanya kazi na mtu yeyote. Na hakuna sehemu ambayo Alikiba amesema sitaki ufanye kazi na msanii huyu wala huyu. Hasemagi na wala hajawahi kuniambia, kwa sababu mimi nije nifanye kazi na mfano labda Diamond, ama Harmonize, Jux ama mtu mwingine nitampa privacy kama nilivyokuwa nampa Alikiba," Producer Yogo alisema.

Leave your comment