Yogo Beats Ajibu Madai ya Kupuuza Wasanii Wengine Alipokuwa Akiandaa Albamu ya Alikiba

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania Producer Yogo Beats amekua gumzo sana baina ya wadau tofauti katika sanaa ya muziki, kutokana na kuwa yeye ndiye producer pekee aliyesuka ngoma zote kumi na sita kwenye albamu ya Alikiba.

Mara mingi wasanii wanapotoa albamu hutumia watayarishaji wa muziki tofauti kwenye ngoma zao. Lakini kwenye albamu ya Alikiba ya 'Only One King', ni Yogo Beats pekee ambaye amehusika katika kutengeneza midundo ya ngoma zote.

Soma Pia: Producer Yogo Beats Asikitishwa Kuona Albamu ya Alikiba Ikiuzwa Mtaani

Kando na wengi kubaki na swali la kwa nini Alikiba alimtumia mtayarishaji wa muziki mmoja tu, madai pia yaliibuka kuwa Producer Yogo alipuuza kazi za wasanii wengine kwa sababu ya albamu ya Alikiba.

Akizungumza katika mahojiano na Wasafi TV, Producer Yogo alisema kuwa wasanii wanaoneza tuhuma hizo wanamkosea sana.

Read Also: Nyimbo Mpya: Alikiba ‘Bwana Mdogo’, Mac Voice ‘Tamu’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Aliongeza kuwa iwapo kuna msanii alihisi kukosewa na yeye, basi angemfuata na amwambie wazi badala ya kuomuongelea kikando. Aidha, Yogo Beats aliongezea kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliokuwa kwenye albamu ya Alikiba, alilazimika kubadilisha mfumo wake wa kufanya kazi.

"Mtu anayekwenda kulalamika kuwa nilishindwa kufanya kazi yake kwa sababu ya albamu ya Alikiba, huyo atakua ameamua kunikosea. Kwa nini asingenifuata mimi personal kuniambia, akaenda kuzungumza kwa watu wengine. Hilo ni kosa, huyo mtu wa namna hiyo siwezi kumzungumzia," Producer Yogo alisema.

Leave your comment