Producer Yogo Beats Asikitishwa Kuona Albamu ya Alikiba Ikiuzwa Mtaani

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Producer Yogo ambaye ndiye mtayarishaji wa muziki rasmi wa msanii Alikiba amesikitishwa na jinsi albamu ya Alikiba inauzwa mtaani na wachuuzi.

Yogo ndiye aliyesimamia utengenezaji wa albamu hiyo ambayo pia iliwahusisha wasanii kutoka sehemu mbali mbali ya bara la Afrika.

Albamu ya Alikiba iliachiwa siku chache zilizopita na imepokelewa vizuri sana na mashabiki na pia kuvuma mtandaoni. Habari zimeibuka kuhusu visa vingi vya wachuuzi kuuza albamu hiyo mitaani kupitia CD, jambo ambalo ni haramu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba ‘Bwana Mdogo’, Mac Voice ‘Tamu’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Akizungumza katika mahojiano na Simulizi na Sauti, Producer Yogo alisema ni jambo la kusikitisha kuwa wauzaji wa albamu hiyo wanapata kipato kutokana na jasho yake na vile vile ya msanii husika ambaye ni Alikiba.

Alieleza kuwa albamu ya msanii hupata pesa mingi sana ila si zote zinazomfikia msanii kutokana na albamu hiyo kusambazwa mtaani na wachuuzi. Kwa mujibu wa Producer Yogo, baadhi ya wasanii hawaishi kiwango cha maisha ambacho wanafaa kwa sababu ya watu wengine kunufaika kutoka kwa albamu zao.

Soma Pia: Collabo Tano Kali Alizofanya Patoranking na Wasanii wa Bongo

Yogo aliongezea kuwa yeye binafsi amepokea taarifa hizo za usambazaji wa albamu ya Alikiba kutoka kwa watu walioko karibu naye. Alikiba hata hivyo sio msanii pekee yake ambaye ameathirika vibaya na usambazaji wa nyimbo zake mtaani.

Yogo alisimulia jinsi amewahi kutana na albamu za wasanii wengi maarufu mtaani ikiwemo; Harmonize, Diamond Platnumz, T.I.D na wengine wengi. Yogo Beats ameiomba serikali kuingilia kati na kuwakinga wasanii dhidi ya athari zinazotokana na usambazaji wa nyimbo mtaani.

Leave your comment