Nyimbo Mpya: Alikiba ‘Bwana Mdogo’, Mac Voice ‘Tamu’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii
15 October 2021
[Picha: Alikiba Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Nchini Tanzania mambo yameendelea kuwa motomoto kwenye kiwanda cha muziki hasa kwenye mtandao wa YouTube ambapo baadhi ya ngoma mpya zilizoachiwa zinaendalea kufanya vizuri. Kwenye nakala hii, tunaangazia ngoma tano ambazo zimefanya vizuri sana kwenye upande wa YouTube:
Soma Pia: Collabo Tano Kali Alizofanya Patoranking na Wasanii wa Bongo
Oya Oya - Alikiba
Ikiwa ni video ya tano kutoka kwenye albamu yake ya ‘Only One King’, ‘Oya Oya’ imeendelea kushika hatamu kwenye mtandao wa YouTube. Kufikia sasa imeshatazamwa mara milioni 2.4.
Tamu - Mac Voice ft Rayvanny
‘Tamu’ ni video ya pili kuachiwa kutoka kwenye EP yake ya ‘My Voice’. Ufundi pamoja na ubunifu wa Eris Mzava kwenye video hii umefanya iwe na viwango vya kimataifa. Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1.3 huko YouTube.
Bwana Mdogo - Alikiba ft Patoranking
Ushirikiano mzuri kati ya Alikiba na Patoranking kuanzia kwenye sauti, mpangilio wa mashahiri umefanya ngoma ya ‘Bwana Mdogo’ iwe kali sana. Ndani ya wiki moja tu tangu kuachiwa, tayari imeshatazamwa mara laki tano arobaini na mbili kwenye mtandao wa YouTube.
Niteke - Alikiba ft Blaq Diamond
‘Niteke’ ni ngoma pendwa sana kwenye albamu ya ‘Only One King’. Mpaka sasa, inaongoza kutazamwa kuliko ngoma yoyote kwenye albamu hii mpya ya Alikiba. Kufikia sasa, imeshatazamwa mara laki tano hamsini na nane kwenye mtandao wa YouTube.
Sina Neno - Jux
Tangu mwanamuziki Jux aachie ‘Sina Neno’ ngoma hii imekuwa ni ngoma ambayo imepokelewa kwa mikono miwili na mashabiki kutokana na mashairi yake kuwa mazuri na yenye kugusa hisia za wengi. Kufikia sasa, imeshatazamwa mara milioni 1.3 kwenye mtandao wa YouTube.
Leave your comment