Nandy Aashiria Kolabo Yake Na Sho Madjozi Kutoka Hivi Karibuni

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Nandy ameashiria kuwa kolabo yake na msanii nyota kutoka Afrika Kusini Sho Madjozi itadondoka hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy alichapisha video ambayo inamwonyesha akisakata densi pamoja na Sho Madjozi. Kwenye video hiyo, Nandy na Sho Madjozi wanaonekana wakiwa studioni huku ngoma waliyokuwa wakicheza ikiwa ya mfumo wa midundo za Amapiano.

Soma Pia: Nandy Atangaza Tarehe ya Ziara Yake ya Muziki Marekani

Taarifa aliyoambatanisha na video hiyo ndiyo iliyoibua hisia kuwa huenda ngoma hiyo ikadondoka hivi karibuni. Bado haijulikani iwapo ngoma waliyokuwa wakicheza ndio ngoma yao ambayo watadondosha ama walikua wakijiburudisha na ngoma tofauti tu.

"Sasaaaa ni muda wa bataa la kunjani…..Weka kama unapenda amapiano!" chapisho la Nandy kwenye ukurasa wake wa Instagram lilisomeka.

Soma Pia: Jux, Nandy Waashiria Ujio wa Kolabo na Patoranking

Aidha hii si mara ya kwanza Nandy kuchapisha video hiyo inayomwonyesha akiwa na Sho Madjozi. Wiki chache zilizopita Nandy alichapisha video hiyo hiyo wakati akidokeza ujio wa kolabo yao.

Chapisho hili jipya la Nandy linatokea siku chache baada ya tetesi kuibuka kuwa huenda ngoma yake na Sho Madjozi ilikuwa imevuja mitandaoni. Nandy na Sho Madjozi, hata hivyo, hawakutoa kauli yao kuhusiana na tetesi hizo.

Kolabo baina ya Nandy na Sho Madjozi inatarajiwa kuwa kubwa mno haswaa ikizingatiwa kuwa wasanii hawa wawili ni wakubwa katika bara la Afrika. Uwezo wa Sho Madjozi kuimba kwa lugha ya Kiswahili pia kutachangia pakubwa katika kuongeza ladha ya ngoma hiyo.

Leave your comment