Nandy Atangaza Tarehe ya Ziara Yake ya Muziki Marekani

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Nandy ametangaza kuwa ataanza ziara ya muziki Marekani mwaka ujao kuanzia tarehe 22 mwezi Machi hadi tarehe 22 mwezi Aprili.

Soma Pia: Jux, Nandy Waashiria Ujio wa Kolabo na Patoranking

Nandy alichapisha tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambako pia aliwasihi mashabiki wake waliokoo Marekani kujiandaa kumkaribisha.

Nandy, hata hivyo, bado hajatoa ratiba ya ziara hiyo. Tangazo hilo limetoka mapema na hivyo basi kuwapatia mashabiki wake kule Marekani wakati wa kutosha kujiandaa.

"USA- March madness 2022 I know you miss me and yess I miss you too. Tukutane baada ya baridi kupita," Nandy aliandika mtandaoni.

Soma Pia: Nandy Azungumzia Changamoto za Kuandaa Matamasha

Nandy amesifiwa sana kwa tamasha yake ya Nandy Festival ambayo huwa anafanya kila mwaka katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania. Tamasha hizo zimempa umaarufu na mafanikio makubwa na huenda ni muda sasa malkia huyo kuvuka mipaka ya Tanzania.

Kwa sasa, Harmonize na Diamond wanaendeleza ziara yao Marekani na wamepata mapokezi mazuri mno. Wawili hao wanapeperusha bendera ya Tanzania na kuuza muziki wa bongo kwa mashabiki wao walioko ng'ambo.

Diamond na Harmonize pia wakiendelea na ziara yao, kwa upande mwingine wanashughulikia albamu zao zinazotengenezewa huko waliko. Mfumo wa wasanii wa kiafrika haswaa kutoka upande wa mashariki kuzuru Marekani kunaashiria kuwa muziki wa kiafrika umeanza kupenya na kuingia katika nchi za kigeni.

Leave your comment