Nandy Azungumzia Changamoto za Kuandaa Matamasha

[Picha: Capital FM]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Nandy amefunguka kuhusu changamoto ambazo amekumbana nazo katika kuandaa matamasha za Nandy Festival.

Nandy amepata umaarufu mkubwa sana kutokana na matamasha yake ya Nandy Festival ambayo huwa anayaandaa kila mwaka. Katika matamasha hayo, Nandy huburudisha katika mikoa mbali mbali nchni Tanzania.

Soma Pia: Nandy Azungumzia Mchango wa Billnass Kwenye Taaluma Yake ya Muziki

Mwaka huu kama vile miaka mingine, Nandy alipata mafanikio makubwa kutokana na Nandy Festival. Nandy aliwaleta wasanii wakubwa kutoka nje ya Tanzania katika matamasha yake. Mmoja wa wasanii wakubwa waliotua Tanzania kwa ajili ya Nandy Festival ni msanii Joe Boy kutoka Nigeria.

Nandy hata hivyo amekiri kuwa si rahisi kuandaa matamasha kwani kuna changamoto mingi sana ikija katika uandalizi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii na Maua Sama, Rosa Ree, Beka Flavor na Wasanii Wengine

"Changamoto zipo kwenye kufanya matamasha kwa mtu yeyote, hata show za kawaida. Hata ma promoter wanajua changamoto lazima ziwepo. Lakini namshukuru mwenyezi Mungu tulianza salama na tumemaliza salama," Nandy alisema.

Nandy amesifiwa na wadau wengi katika tasnia ya muziki nchini Tanzania kutokana na mafanikio ya Nandy Festival. Msanii mwingine ambaye pia amesifiwa hivi karibuni kutokana na mafanikio ya tamasha lake ni Zuchu.

Zuchu alianda tamasha lake la Zuchu Homecoming lilifanyika mkoani Zanzibar. Tamasha hilo lilivutia mamia ya watu ambao walifurika uwanjani kuja kuburudika. Wasanii hutumia tamasha kama mojawapo ya njia ya kupata kipato. Tamasha zinapopata mafanikio ina maana kuwa msanii huyo aliyeandaaa atapata kipato kikubwa.

Leave your comment