Abby Chams Azungumzia Tetesi za Kujiunga na Next Level Music ya Rayvanny

[Picha: Abby Chams Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msani tajika kutokea Tanzania Abby Chams hatimaye amezungumzia tetesi zilizopo baina ya mashabiki kuhusu yeye kujiunga na lebo ya Rayvanny ya Next Level Music.

Tetesi za Abby Chams kujiunga na lebo ya Next Level Music zilipamba wiki kadhaa nyuma baada ya msanii huyo kuonekana akiwa studio za Next Level Music na Rayvanny, hivyo mashabiki wengi kujumuisha kuwa huenda Abby Chams ameshajiunga na Lebo hiyo.

Soma Pia: Baba Levo Azungumzia Tetesi za Hanstone Kuondoka WCB

Akiongea kwenye mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha redio cha Times FM, Abby Chams ameeleza kuwa picha alizopiga na Rayvanny hazina uhusiano wowote na yeye kujiunga na lebo hiyo, kwani walikuwa wanarekodi tu nyimbo pamoja.

"Zile picha ambazo zilisambaa nilikuwa narekodi nyimbo, nimerekodi nyimbo na Rayvanny so I think people they saw those and then they just assumed, so thats what happened. Hizo picha they had nothing to do with signing," alizungumza Abby Chams.

Soma Pia: Ibraah Azungumzia Ziara ya Muziki ya Harmonize Kulinganishwa na Ile ya Diamond

Kwa sasa, Abby Chams anatamba na ngoma yake ya kuitwa ‘Tucheze’ ambayo aliitoa siku kadhaa zilizopita. Kufikia sasa, Abby ameshafanya kazi na wasanii wakubwa nchini Tanzania kama Darassa pamoja na Mimi Mars.

Leave your comment