Ibraah Azungumzia Ziara ya Muziki ya Harmonize Kulinganishwa na Ile ya Diamond

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii wakubwa nchini Tanzania Harmonize na Diamond Platnumz kwa sasa wako Marekani kwa ziara tofauti za kimuziki.

Harmonize ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika Marekani na kuanza ziara yake kisha baadae Diamond Platnumz akafika huko na pia kuanzisha yake.

Soma Pia: Ibraah Akana Madai ya Kuwa na Ugomvi na Wasanii wa Bongo

Wasanii hawa wawili wanapoendelea na ziara yao kwa wakati mmoja, kumekuwa na ushindanishi mkubwa katika mitandao ya kijamii. Japo wawili hawa walipata mapokezi mazuri, mjadala wa nani amepata mafanikio zaidi ya mwingine umezidi kuvuma mtandaoni.

Msanii Ibraah kutoka lebo ya Konde Gang ambayo inamilikiwa na Harmonize amefunguka kuhusu ushindanishi huo. Ni muhimu kutaja kuwa Ibraah pia alikuwepo Marekani na kutumbuiza katika baadhi ya maonyesho kwenye ziara ya Harmonize.

Kwa mujibu wa Ibraah, watu wako na uhuru wa kuwa na mjadala wowote wanaotaka ikiwemo kuwashindanisha wasanii. Aliongezea kuwa wao hawawezi kumkataza mtu yeyote kuchapisha maoni yake ata kama inawagusa.

Soma Pia: Maud Elka Aashiria Uwezekano wa Kolabo Baina yake na Ibraah, Diamond

"Mimi simkatazi mtu kuoniongelea katika angle ambaye yeye anahisi ni sahihi kuniongelea. Alafu hauwezi kumpangia mtu na ndio iko hivyo duniani kote. Na watu wangekosa kuongea ni na imani kuwa tusingefikia huko," Ibraah alisema.

Ibraah alikuwa akizungumza baada ya kuulizwa kauli yake kuhusu mjadala huo. Ibraah vile vile aligusia suala la tetesi zilizoibuka mtandaoni kuwa huenda ziara ya Harmonize haikupata mafanikio makubwa.

Leave your comment