Maud Elka Aashiria Uwezekano wa Kolabo Baina yake na Ibraah, Diamond

[Picha: Maud Elka Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Maud Elka kwa sasa yupo nchini Tanzania kwa kazi ya muziki.

Sababu kuu iliyomleta Maud Elka Tanzania ni uzinduzi wa albamu ya Alikiba. Wasanii hawa wawili walitoa kolabo ya 'Song Songi remix' ambayo ilipokelewa vizuri sana na mashabiki.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Tarehe ya Uzinduzi Rasmi ya Albamu Yake ‘Only One King’

Akizungumza na wanahabari alipotua katika uwanja wa ndege, Maud alisema kuwa kuna uwezekano wa yeye kufanya kazi na wasanii wengine wa bongo. Aliwataja Ibraah na Diamond kama wasanii ambao huenda akafanya kazi nao ila hakutoa habari zaidi kuhusiana na maandalizi ya kolabo hizo.

Maud aliongezea kuwa atakuwa akitumbuiza katika tamasha mbali mbali Tanzania kuanzia hii wikendi.

"I am here to do some shows on the next days, on this weekend and I hope I will be doing other shows the next week. So maybe there is a shooting maybe not," Maud Elka alisema.

Soma Pia: Nandy, Patoranking Waingia Studio Nchini Zanzibar

"There is a lot of really talented artists here. I have been contacted so am gonna see. There is Ibraah, Diamond, a lot of artists that I like, really," aliongezea.

Maud Elka pia alisema kuwa alifurahia mapokezi ambayo wimbo wake wa 'Songi Songi' ulipata nchini Tanzania. Kwa mujibu wa msanii huyo, alipata kumjua Alikiba kupitia rafiki yake ambaye pia alimtambulisha kwake, na baada ya hapo wawili hao wakaingia studioni na kutengeneza 'Songi Songi' remix.

Leave your comment