Alikiba Atangaza Tarehe ya Uzinduzi Rasmi ya Albamu Yake ‘Only One King’

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki Alikiba ametangaza rasmi tarehe ya uzinduzi wa albamu yake ambayo kwa sasa ndio gumzo katika tasnia ya muziki ya Tanzania.

Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, albamu hiyo hatimaye itatoka tarehe saba mwezi huu. Ila kabla ya kutoka kwake, Alikiba ameandaa uzinduzi wake tarehe sita.

Hafla hiyo itahudhuriwa na waalikwa pekee ambao watapata fursa ya kuzisikiliza ngoma zilizoko kwenye albamu hiyo.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Jina na Siku Atakayoachia Albamu Yake Mpya

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba ametangaza kuwa siku ya Jumatano ambayo ni tarehe sita atajumuika na wadau tofauti kabla ya kuiachia albamu yake sikua ifuatayo.

"Kama nilivyosema awali tarehe 6 Oktoba nitakua na Hafla ya kipekee Kabisa, nitajumuika na Wadau mbalimbali katika Uzinduzi wa Album yangu "ONLY ONE KING".Je! wewe ni mmoja wa waalikwa?" ujumbe wa Alikiba mtandaoni ulisomeka.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu ya Kutofanya Swahili Amapiano Licha ya Umaarufu wa Mtindo Huo

Kwa sasa, Alikiba anaendelea kuwatambulisha baadhi ya waalikwa wa uzinduzi wa albamu yake. Waliotajwa kufikia sasa kama wageni waalikwa ni malkia wa muziki wa bongo Nandy, muigizaji na mwana mitindo Wema Sepetu na msanii wa mtindo wa Hip-hop Mwana FA.

Albamu hiyo inatarajiwa kutikisa anga ya burudani kwani ni ya kipekee na imewahusisha wasanii wengine wakubwa kutoka pande tofauti ya Afrika.

Leave your comment