Ibraah Akana Madai ya Kuwa na Ugomvi na Wasanii wa Bongo

[Picha: Mtikiso Entertainment]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ibraah hatimaye amefunguka kuhusu madai ya uhasama baina yake na wasanii wengine nchini Tanzania. Kwa muda sasa uvumi umesambaa mtandaoni ukiashiria kuwa huwenda Ibraah hayupo katika hali ya mazungumzo na wenzake kutoka bongo, haswaa wale kutoka lebo nyingine mashuhuri.

Soma Pia: Ibraah Aeleza Sababu ya Kuchelewa Kuachia Wimbo Mpya

Hapo awali, Ibraah alitoa wimbo unaoitwa 'Hayakuhusu' ambapo aliwasomea wasanii wenzake wa bongo haswaa wale walio na utaofauti na Harmonize. Ngoma hiyo iliibua gumzo sana miongoni mwa mashabiki.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Ibraah alifunguka na kusema kuwa hana ugomvi na msanii yeyote kutoka nchini Tanzania. Aliongeza kuwa amekuwa akiwashabikia wasanii wengi waliomtangulia.

"Mimi sina ugomvi na msanii yeyote Tanzania," Ibraah alisema.

Soma Pia: Harmonize Ampongeza Ibraah Baada ya Wimbo Wake ‘Jipinde’ Kuvunja Rekodi

Aidha, Ibraah aliendelea kwa kusema kuwa sio vyema wasanii kuwachukia wenzao pasipo na sababu. Alizungumzia suala la msanii Baba Levo ambaye amejulikana kwa kuwa mkosoaji wa Harmonize na mtetezi wa Diamond.

"Huyo ana chuki, na chuki sio nzuri wangwana. Usinichukie pasipo na sababu maanake mimi sijakukosea wewe," Ibraah alisema.

Kwa sasa, Ibraah anatamba katika anga za burudani kupitia wimbo wake wa ‘Jipinde’ uliomletea mafanikio makubwa. ‘Jipinde’ uliandikisha rekodi ya kupata watazamaji milioni moja ndani ya masaa kumi na tano, na kuwa wimbo wa kwanza wa Ibraah kupata watazamaji wengi ndani ya muda mfupi.

Leave your comment