Ibraah Aeleza Sababu ya Kuchelewa Kuachia Wimbo Mpya

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika Ibraah kutokea lebo ya Konde Music Worlwide hatimaye amefunguka kuhusu ukimya wake wa muda mrefu kwenye muziki. Hapo awali, ukimya wa Ibraah wa miezi mingi sana ulikuwa umeibua maswali huku wengi wakijiuliza ni lini angetoa wimbo wake mpya.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Ibraah alieleza kuwa yeye kama msanii alieye chini ya lebo ya Konde Worldwide alikuwa anafuata ratiba iliyowekwa na usimamizi wa lebo hiyo.

Soma Pia: Wimbo Mpya wa Ibraah 'Jipinde' Wamuandikishia Rekodi Mpya

Aliongeza kuwa usimamizi wa lebo hiyo ndiyo inayoelekeza matendo yake kimuziki na hivyo basi hao ndio wa kuamua wakati mwafaka wa yeye kutoa ngoma.

Aidha Ibraah alisifia usimamizi wa Konde Worldwide kwa kuwa wenye hekima na busara katika uamuzi wao. Kulingana na Ibraah, uongozi wa Konde Music hawakurupuki katika mikakati yao ya kuachia miziki.

Soma Pia: Harmonize Ampongeza Ibraah Baada ya Wimbo Wake ‘Jipinde’ Kuvunja Rekodi

"Ni kwa mipangilio na kwa sababu hamna kampuni ambayo haina mipango. Na naushukuru sana uongozi wa Konde Music kwa sababu una uongozi mwema. Siku zote naonanga wako sahihi kwa sababu hawakurupuki. wanajua utafanya project yako hii, utafanya hii na still utakuwa uko hapa. Na ndio huyu mimi niko hapa," Ibraah alisema.

Ibraah pia alijibu mashabiki wanaomlinganisha na Harmonize kwa kusema kuwa Harmonize kamwe ni mkubwa wake na hatoweza kumpiku kimuziki.

Leave your comment