Harmonize Ampongeza Ibraah Baada ya Wimbo Wake ‘Jipinde’ Kuvunja Rekodi

[Picha: SoundCity TV]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize amempongeza msanii Ibraah kwa mafanikio aliyoyapata kimuziki hivi karibuni.

Ibraah ambaye amesainiwa katika lebo ya Harmonize, amejiandikishia rekodi mpya baada ya ngoma yake ‘Jipinde’ kupata watazamaji milioni moja ndani ya masaa kumi na tano kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Wimbo Mpya wa Ibraah 'Jipinde' Wamuandikishia Rekodi Mpya

Kwenye ujumbe aliyouchapisha mtandaoni, Harmonize alimpongeza Ibraah kwa kusimama imara katika muziki licha ya kupitia changamoto mingi. Kulingana na Harmonize, wapo wengi waliojaribu kumkatisha Ibraah tamaa katika safari yake ya muziki.

Harmonize aliongeza kuwa sasa ulikuwa umewadia wakati wa nyota ya Ibraah kung'aa katika tasnia ya muziki ya Tanzania.

"Congrats my brother @ibraah_tz  it's your time now kuwashukuru wote waliokukatishaga tamaa ...!!! na kukumbuka yale magumu uliyoyapitia na kuyahesabu kama zilikuwa changamoto ilii uuone ukuu wa Mungu ...! Go go go ...! Keep going and make the team proud (1.m) b4 the day #Kondegang4you run it up my people," ujumbe wa harmonize ulisomeka mtandaoni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia ‘Jipinde’

Ibraah kwa upande mwingine akizungumza katika mahojiano na Simulizi Na Sauti alimshukuru Harmonize kwa kumuunga mkono. Aidha, aliongeza kuwa Harmonize hakuwahi kata tamaa na yeye licha ya kukumbana na ugumu mwingi ambao ungemkatisha tamaa.

Aliongeza kuwa wakati wake wa kupaa katika muziki umefika na kamwe hana chuki na wale waliojaribu kukatisha ndoto yake ya muziki. Ibraah amependwa na wengi sana kutokana na mtindo wake wa kuimba na ustadi katika mistari ya nyimbo zake.

Leave your comment