Wimbo Mpya wa Ibraah 'Jipinde' Wamuandikishia Rekodi Mpya

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Ibraah anayekua kwa kasi sana katika tasnia ya muziki ya Tanzania kwa sasa anavuma kwenye anga za burudani na ngoma yake mpya ‘Jipinde’.

Ngoma hiyo iliyoachiwa tarehe 18 mwezi Agosti imemuandikishia Ibraah rekodi mpya katika taaluma yake ya muziki. ‘Jipinde’ imengia kwenye rekodi kama nyimbo ya Ibraah iliyopata watazamaji wengi sana kwenye YouTube ndani ya muda mchache.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia ‘Jipinde’

Ngoma hiyo ilivutia watazamaji takriban milioni moja ndani ya masaa kumi na tano tu. Wengi wa watazamaji wamependezwa na ubora wa wimbo hiyo na vile vile mtindo ambao Ibraah ameutumia kuimba.

Kwenye ngoma hiyo, Ibraah anasifia urembo wa mwanadada ambaye yumo naye kwenye mahusiano.

"Moja nikusifie we kama katuni mwendo hauna kasoro, na kawimbo ni kuimbie sio kwa mafumbo kweli mwali mwali nimefollow shida ya upendo," Ibraah aliimba kwenye wimbo wake mpya.

Soma Pia: Khadija Kopa Asimulia Sauti Ilvyompotea Akiwa Jukwaani Akashindwa Kuimba

Aidha, Ibraah alichapisha mtandaoni ujumbe wa shukrani kwa mashabiki wake kwa kumuunga mkono na kumwezesha kupata watazamaji milioni moja ndani ya muda mfupi.

 "Happy 1m viewers. Nakubaliana na ninyi watu wangu wa nguvu. Leo nitakunywa soda na ma vyakula hadi nivimbiwe nikimaliza na nunua bambino nisije nikalibwaga kitandani," ujumbe wa Ibraah ulisomeka.

Ibraah ni mmoja wa wasanii chipukizi wanaofanya vizuri sana kutokea lebo ya Konde Music Worldwide.

Nyimbo zake hupokelewa vizuri na mashabiki na tayari ashapata umaarufu ndani na nje ya Tanzania.

Leave your comment