Rapcha Azungumza Baada ya Profesa Jay Kumfananisha na Mangwair

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Rapcha amefunguka ya moyoni baada ya rapa Profesa Jay kufananisha aina yake ya muziki na ile ya marehemu Albert Mangwair.

Kupitia akaunti yake ya Instagram siku mbili zilizopita, Professa Jay alimpongeza Rapcha kwa muziki mzuri anaoufanya na kumfananisha na marehemu Albert Mangwair.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mac Voice Aachia Video Mpya 'Pombe' Akiwashirikisha Rayvanny na Leon Lee

 "Huyu Dogo ananikumbusha uwezo mkubwa sana wa marehemu Albert Mangwair wa kipaji kikubwa cha kuweza kuimba na kuchana kwa mpigo. Namuona mbali sana," aliandika Profesa Jay.

Akiongea na kituo cha Times FM, Rapcha amemshukuru sana na Profesa Jay kwa kuamini kipaji chake kiasi cha kumfananisha na Mangwair na ameahidi kufanya kazi nzuri zaidi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Cheed Aachia Ngoma Mpya ‘Final’

"Hii ni call ya kunikumbusha kwamba mimi ni nani na nina kitu gani ndani yangu na nnahitaji kukipeleka wapi. Enough respect kwa yeye kuweza kutake time yake. Mi naapreciate sana hicho kitu," alizungumza Rapcha.

Uwezo wa Rapcha kwenye muziki wa Rap unaonekana zaidi kwenye albamu yake ya ‘Wanangu 99’ ambayo imesheheni ngoma 10. Ukisikiliza ngoma ‘Nitakucheki’ au ‘Kama Unae’, uwezo wa Rapcha unaonekana vilivyo. Rapcha yuko chini ya lebo ya mtayarishaji wa muziki nguli kutokea Tanzania P Funk Majani ambaye ana wasifu wa kufanya ngoma na wasanii wakubwa Bongo kama Mangwair, Professa Jay, Fid Q na wengineo wengi.

Leave your comment