Nyimbo Mpya: Cheed Aachia Ngoma Mpya ‘Final’

[Picha: Muziki TZ]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Cheed kutokea label ya Konde Music Worldwide ameachia ngoma mpya kabisa inayoitwa ‘Final’.

Cheed ambaye wiki chache nyuma alichangamsha Tanzanian na ngoma yake ya ‘Wandia’, anabadilika kidogo kwenye ‘Final’ ambayo anatumia sauti yake nzuri kukiri mbele ya mpenzi wake jinsi anavyompenda kwa dhati.

"Nyuma ka kaficha maboga huko, nakafundisha kupiga Yoga iko katoto kamenikoroga hako katoto kamenivuruga hivyo," anaimba Cheed kwenye aya ya kwanza ya ngoma hii.

Tofauti kabisa na kwenye ‘Wandia’, ndani ya ngoma hii Cheed anaimba kwenye mdundo wa kuchangamka na ni ngoma ambayo inatarajiwa kurindima haswaa kwenye club na sehemu tofauti za starehe.

Soma Pia: Cheed Aeleza Chanzo Cha Ukimya Wake Tangu Ajiunge na Konde Gang

Terriyo Monster ndiye amehusika kuandaa ngoma hii na pia ndiye aliyehusika kuandaa ngoma yake ya Cheed ya kwanza chini ya Konde Gang ‘Wandia’ na ‘Roho’ ya msanii Killy.

‘Final’ ni ngoma ya pili ya msanii Cheed chini ya lebo ya Konde Gang na hivi karibuni alifunguka kuwa alikaa kimya kwa takriban mwaka mmoja na miezi kadhaa kwa sababu alikuwa anaandaa albamu yake ambayo iko mbioni kuingia sokoni.

Wimbo huu bado hauna video rasmi ila matarajio ni hivi karibuni kama alivyofanya kwenye ‘Wandia’.

https://www.youtube.com/watch?v=4gTujLSfEiI

Leave your comment

Top stories

More News