Harmonize Atangaza Tarehe Cheed Ataachia Ngoma yake ya Pili Chini ya Konde Gang

[Picha: Muzik TV]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza tarehe rasmi ambayo msanii Cheed aliyesainiwa katika lebo hiyo ataachia wimbo wake wa pili.

Cheed ndiye msanii mpya zaidi ambaye ametambulishwa kutoka lebo ya Konde Music na hivi karibuni aliachia wimbo wake uliopewa jina la 'Wandia'.

'Wandia' umepokelewa vizuri na mashabiki na kufikia sasa umepata zaidi ya watazamaji laki mbili kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Mac Voice, Cheed, Barnaba na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

Kwa mujibu wa Harmonize, Cheed atadondosha wimbo wake wa pili tarehe 15 mwezi huu. Harmonize hata hivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na jina ya wimbo hiyo.

"My brother jus told me dat his dropping anada one ..!! Friday who is ready ...?” chapisho la Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram lilisomeka.

Lebo ya Konde Music Worldwide kwa sasa inamfanyia Cheed kampeni ya kumtambulisha na kama msanii wao mpya. Cheed alitambulishwa rasmi mwaka jana kama mwanachama wa Konde Music ila hakuwa ametoa ngoma yoyote chini ya lebo hiyo.

Soma Pia: Cheed Aeleza Chanzo Cha Ukimya Wake Tangu Ajiunge na Konde Gang

Kabla ya kujiunga na lebo ya Harmonize, Cheed pamoja na mwenzake Killy walikuwa wanachama wa lebo ya Kings Music inayomilikiwa na Alikiba. Killy alishatambulishwa na tayari ameshatoa ngoma kadhaa ambazo zimempa umaarufu hata zaidi kwenye lebo hiyo.

Kwa sasa, Cheed anazidi kutamba kwenye anga za burudani kupitia wimbo wake wa 'Wandia'.

Leave your comment

Top stories

More News