Rais Samia Suluhu Awapongeza Wasanii wa Bongo Waliotajwa Kuwania Tuzo za AFRIMA

[Picha:YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu ametoa pongezi kwa wasanii sita kutokea Tanzania ambao wametajwa kuwania tuzo za AFRIMA mwaka huu wa 2021.

Rais Samia alitoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya virusi vya Covid-19 huko mkoani Dodoma.

Soma Pia: Sababu Nne Kuu Zinazowafanya Wasanii Wengi Tanzania Kuanzisha Lebo za Muziki

Rais aliwapongeza wasanii hao na aliwahasa watanzania wawapigie kura kwa wingi ili waweze kushinda.

"Ninawapongeza wasanii sita ambao wameingia fainali za Tuzo za AFRIMA za Marekani katika vipengele mbalimbali. Wasanii hao ni Diamond Platnumz, Alikiba, Nandy, Zuchu, Marioo na Rosa Ree na muda ukifika tukawapigie kura," alizungumza Rais Samia.

AFRIMA ni tuzo ambazo huandaliwa na kamati ya kimataifa ya AFRIMA wakishirikiana na Umoja wa Afrika (AU). Tuzo hizo zilianza rasmi mwaka 2014 na kufikia sasa wasanii tofauti tofauti kutokea Tanzania wameshinda kama vile Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy, Vanessa Mdee, Harmonize, Lady Jaydee na wengineo wengi. Mwaka huu tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika November 14.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba ‘Oya Oya’, Mac Voice ‘Tamu’ na Ngoma Zingine Zinazotamba Bongo Wiki Hii

Pongezi hizi zinakuja kipindi ambacho kumekuwa na mjadala usioisha kwenye uwanja wa Bongo Fleva kuhusu kukosekana kwa tuzo muziki nchini Tanzania kwa takriban miaka sita sasa tangu tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards kusitishwa mwaka 2015.

Leave your comment