Nyimbo Mpya: Alikiba ‘Oya Oya’, Mac Voice ‘Tamu’ na Ngoma Zingine Zinazotamba Bongo Wiki Hii

[Picha:YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Imekuwa ni wiki nzuri sana kwenye kiwanda cha muziki hapa Tanzania kwani ngoma kutoka kwa wasanii tofauti zimeendelea kufanya vizuri hasa kwenye mtandao wa YoutTube. Makala hii imelenga kuangazia ngoma tano ambazo zinafanya vizuri zaidi hapa Tanzania kwenye mtandao YouTube:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Hatimaye Aachia ‘Only One King’ Album

Oya Oya – Alikiba

Mara tu baada ya kutambulisha albamu yake ya ‘Only One King’, Alikiba aliachia video ya ‘Oya Oya’ ambayo inaonesha upande wa pili ya msanii huyo kwenye kucheza dansi. Video ya ‘Oya Oya’ imeandaliwa na Kylie White. Ndani ya siku moja tu, video hio imeshatazamwa mara laki tano themanini na mbili elfu.

https://www.youtube.com/watch?v=HiX-aYj2yas

Sina Neno - Jux

Jux ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya’Sina Neno’ ambapo anampongeza mpenzi wake wa zamani kwa kupata ujauzito, huku akiendelea kusisitiza kuwa hana tatizo nae kabisa. Video ya ngoma hii imeongozwa na Hanscana na kufikia sasa imeshatazamwa mara milioni moja nukta mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=cDxZrTIcKLk

Bwana Mdogo - Alikiba ft Patoranking

‘Bwana Mdogo’ ni ngoma namba tisa kwenye albamu ya ‘Only One King’. Kwenye ngoma hii, Alikiba anasheherekea na kufurahi mahusiano aliyokuwa nayo kwa kumsifia mpenzi wake. Mdundo mzuri kutoka kwa Yogo Beats bila shaka utafanya ngoma hii kuwa ngoma pendwa kwenye clubs na sehemu mbalimbali za starehe.

https://www.youtube.com/watch?v=bmPIjtnY3iA

Niteke - Alikiba ft Blaq Diamond

Ngoma ya ‘Niteke’ aliyomshirikisha Blaq Diamond kutoka Afrika kusini ni kielelezo tosha kuwa albamu ya Alikiba ni ya moto sana. Kwenye ngoma hii, Alikiba anamuomba mpenzi wake aendelee kumzidishia dozi ya mapenzi. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara laki mbili arobaini na nne kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=CPfxfbzZRXY

Tamu - Mac Voice ft Rayvanny

Mac Voice hatimaye ameachia video ya ngoma yake ya ‘Tamu’ aliyomshirikisha Rayvanny. Ndani ya muda mfupi tu tangu kuachiwa kwake, watanzania wameipokea video hiyo kwa mikono miwili kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara laki nne kumi na moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=3mlDNZRkX6I

Leave your comment