Tommy Flavour Afunguka Jinsi Alivyopata Kolabo na Alikiba Katika Wimbo 'Jah Jah'

[Picha: Alikiba/Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipukizi kutoka Kings Music Tommy Flavour amefunguka kuhusu jinsi alivyopata kolabo na mwanamuziki nyota Alikiba kwenye wimbo wa 'Jah Jah'.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Tommy Flavour alidai kuwa ni ngumu sana msanii yeyote kumshawishi Alikiba kuingia katika kolabo.

Soma Pia: Tommy Flavour Awasifu Harmonize, Diamond Kwa Kupeperusha Bendera ya Tanzania Kimuziki

Kauli ya Tommy Flavour ina ukweli mkubwa kwani Alikiba mwenyewe wakati akitangaza albamu yake rasmi alikiri kuwa ni nadra sana yeye kufanya kolabo. Tommy Flavour alieleza kuwa alikuwa ameuandika wimbo wa 'Jah Jah' na ngoma hiyo haikuwa imepangwa kuwa kolabo.

Ila, Alikiba aliusikiza wimbo huo na akapendezwa nao na hivyo basi akajitolea kufanya kolabo na Tommy Flavour kusudi amshike mkono na kumsaidia kupanda ngazi ya muziki.

Soma Pia: Tommy Flavor Afichua Sababu ya Kuandika Ngoma ya ‘Jah Jah’

"Unajua brother Kiba ni vigumu sana kumshawishi apende kitu, huwaga anapenda yeye mwenyewe. Ni yeye itoke moyoni kwanza ndio aipende. So Kwenye Jah Jah ilikuwa ni hivyo. Niliifanya na akatumiwa na akaipenda. And then baada ya muda akaja akaniambia kuwa Tommy nimeipenda hii kazi, nafikiri tufanye kitu pamoja niku support mdogo wangu. Kwa hiyo mimi nachukulia kama kitu kikubwa kwa sababu sio kitu rahisi kumpata Ali na kufanya na yeye kazi kwa mpigo namna hii. Kwa hiyo ni kitu kikubwa namshukuru," Tommy Flavour alisema.

Ngoma ya 'Jah Jah' ambayo ni ya kumtukuza Mungu imepokelewa vyema na mashabiki. Ngoma hiyo imepata zaidi ya watazamaji nusu milioni ndani ya takriban siku sita.

Leave your comment