Nyimbo Mpya: Mac Voice Aachia Video ya 'Nenda'
29 September 2021
[Picha: DJ Chepe]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Msanii chipukizi Mac Voice kutoka lebo ya Next Level Music ameachia video ya wimbo wake wa 'Nenda'.
'Nenda' ni wimbo ambao unazungumzia maumivu ambaye mhusika mkuu kwenye video, Mac Voice, anapitia baada ya kuachwa na mpenzi aliyempenda kwa dhati.
Soma Pia: Mac Voice Aratibiwa Kuanza Media Tour ya Kwanza Chini ya Next Level Music
Tofauti na hali ya kawaida ambapo aliyeachwa hubaki na maumivi kiasi cha kumchukia mwenziwe, Mac Voice kwenye wimbo huu anamtakia mema mrembo aliyemwacha licha ya maumivu ya roho anayopitia.
"Mapenzi niliyaanzisha yakanifurahisha yakanibadilisha jamani, Na sio to kumridhisha nikamdhaminisha, nikamtamulisha nyumbani. Sasa leo yamekwisha yananidhalilisha yananiaibisha hadharani ila yote ni maisha, japo nahuzunika eeh wa kuninyamazisha ni nani? Sijuti kukufahamu, ila najuta kukuamini Kasuku nclege wangu leo umekuwa bundi Pokea zangu salamu, badO sijui nitapona lini? Umevunja moyo yangu, we ndo ulikuwa gundi..." Mac Voice anaimba kwenye 'Nenda'.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mac Voice Aachia EP Mpya ‘My Voice’ Chini ya Next Level Music
Ngoma hii ya 'Nenda' imetayarishwa na mmoja wa watayarishaji wa miziki wanaoheshimika sana Tanzania naye ni Lizer Classic kutoka lebo ya WCB. Lizer Classic ni mtayarishaji wa miziki ambaye amefanya kazi na wasanii wakubwa sana Afrika, na uwepo wa ufundi wake uliufanya 'Nenda' kuwa ngoma yenye ubora wa hali ya juu.
Utayarishaji wa video kwa upande mwingine umesimamiwa na Next Level Music. Manthari ya video inavutia mno na yenye hadhi yake. Kama vile ujumbe uliopo kwenye ngoma, Mac Voice anaonekana kwenye video akivurugana na mpenzi wake ambaye baadaye anamwacha na kumwendea mwanaume mwingine ambaye ni tajiri zaidi.
'Nenda' imepokelewa vyema sana na mashabiki na tayari ishapata maelfu ya watazamaji ndani ya muda mfupi.
Leave your comment