Mac Voice Aratibiwa Kuanza Media Tour ya Kwanza Chini ya Next Level Music

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Lebo ya Next Level Music chini ya usimamizi wa mwanamuziki nyota Rayvanny imezidisha kampeni za kumtabulisha msanii wao mpya Mac Voice.

Lebo hiyo ilimtambulisha rasmi Mac Voice kama msanii wa kwanza chini ya usimamizi wake siku kadhaa zilizopita.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mac Voice Aachia EP Mpya ‘My Voice’ Chini ya Next Level Music

Baada ya kuachia EP iliyopokelewa vizuri sana na mashabiki, Mac Voice kwa sasa ameratibiwa kuanza 'media tour' ambayo itawapa mashabiki fursa ya kumjua zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny alitangaza 'media tour' hiyo huku akiwashukuru mashabiki kwa mapokezi mazuri waliyomwonyesha Mac Voice.

Rayvanny aliwaomba mashabiki pamoja na wadau wengine kwenye tasnia ya muziki kuendelea kumshika mkono Mac Voice katika safari yake ya muziki.

Soma Pia: Rayvanny Ashauri Msanii Wake Mpya Mac Voice Jinsi ya Kufanikiwa Kimuziki

"Kwanza nianze Kwa kushukuru Kwa mapokezi yenu makubwa. Media zote TV, Radio, Magazeti, Blogs lakini pia online TVs Na vituo vyote vya habari Kwa kumpokea kijana wenu lakini pia kushare kila kinachomuhusu Kwa jamaii. Kuanzia sasa tutajumuika nanyi ikiwa ni utambulisho wa kijana wenu @macvoice_tz kikubwa tunaomba sapoti nasi hatutawaangusha," ujumbe wa Rayvanny mtandaoni ulisomeka.

Kwa sasa mashabiki wanaendelea kuburudika na ngoma ambazo Mac Voice ameachia kupitia EP yake ambayo iko na nyimbo sita. Nyimbo hizo ni; Nenda, Mama Mwenye Nyumba, Nampenda, Tamu, Bora Pekee Yangu na Pombe.

Nyimbo hizo zimehusisha majina kubwa kwenye tasnia ya muziki wakiwemo watayarishaji wa miziki wenye hadhi ya juu kama vile Lizer Classic na S2kizzy. Rayvanny pia amehusika pakubwa kwani ameshirikishwa katika baadhi ya nyimbo.

Leave your comment