Rayvanny Ashauri Msanii Wake Mpya Mac Voice Jinsi ya Kufanikiwa Kimuziki
20 September 2021
[Picha: Cyclone Times]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mkuregenzi mkuu wa lebo ya Next Level Music Rayvanny amemshauri msanii wa kwanza ambaye amesainiwa chini ya lebo hiyo Mac Voice jinsi ya kufanikiwa kimuziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny alimshauri Mac Voice kuzingatia Mungu, heshima na bidii.
Soma Pia: Rayvanny Amtambulisha Msanii wa Kwanza wa Next Level Music
"Mungu alikupa kipaji ili kikusaidie na kwenye maisha ni muhimu kuzingatia mambo haya! 1.Mungu 2.Heshima 3.Bidii Utayaona mafanikio ukizingatia hayo zaidi ni wadau na wapenzi wamuziki ( mashabiki) kumsapoti kijana wenu ili kesho Na kesho kutwa nae awasaidie wengine!" chapisho la Rayvanny lilisomeka.
Rayvanny alimtambulisha msanii Mac Voice wikendi iliyopita. Kwa sasa, yeye ndio msanii wa kwanza aliyenasijiliwa na lebo hio.
Inakisiwa kuwa msanii Mac Voice atazinduliwa rasmi au kuachia kazi yake ya kwanza tarehe ishiri nan ne mwezi huu.
Kwa wafuatiliaji wa muziki nchini Tanzania, Mac Voice ni msanii ambaye kabla ya kusainiwa na Rayvanny alikuwa ameshatoa ngoma kadhaa huko nyuma na kuna kipindi alikuwa na ukaribu na msanii Chege na walitoa ngoma tofauti tofauti kama vile ‘Utarudi’, ‘Mama J’ na ‘Damu ya Ujana’.
Baada ya ngoma hizo kufanya vizuri, Mac Voice alikaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa wimbo mpaka siku ya leo alivyotambulishwa rasmi kama msanii wa Rayvanny chini ya Next Level Music.
Kwa sasa, macho na masikio yapo hapo Next Level Music ili kujua Mac Voice ameaandaa kitu gani kwa mashabiki.
Leave your comment