Alikiba Awapa Mashabiki Nafasi Kuchagua Jina la Albamu Yake

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Alikiba amewapa mashabiki wake nafasi ya kuchagua jina la albamu yake ambayo anatarajiwa kuachia hivi karibuni.

Hii inatokea muda mfupi baada ya Alikiba kutangaza kukamilika kwa album hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba alifichua kuwa amekuwa akiwaza ni jina lipi ataipa albamu yake ila bado hajafikia uamuzi.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Kukamilika kwa Albamu Yake

Hivyo basi aliona ni jambo zuri kuhusisha mashabiki wake katika uamuzi huo. Aliwaelekeza mashabiki wake kupendekeza jina la albamu yake kupitia sehemu ya maoni ya chapisho hilo mtandaoni. Aliahidi kuwa atachagua jina bora kutoka kwa majibu yaliyopendekezwa.

"Mashabiki Zangu Nimekua nikifikiria jina gani litafaa kuipa Album Yangu mpya.Nadhani Hii ni Challenge kwenu sasa, Pendekeza jina la Album Comment Kwa #Hashtag Na nitachagua bora zaidi," chapisho la Alikiba mtandaoni lilisomeka.

Aidha, Alikiba pia alitangaza kuwa atakua na kikao na wanahabari mnamo tarehe 29 mwezi huu.

Soma Pia: Alikiba Apokea Tuzo Mbili Kutoka YouTube

"Habari Napenda Kuwaalika Waandishi wote wa Habari Siku ya Kesho Pale Hyatt Regency Hotel Kuanzia Saa 11:00Am Asubuhi (East Africa Time) muhimu sana Nawakaribisha wote," Alikiba aliandika mtandaoni.

Bado haijabainika iwapo Alikiba atafichua tarehe kamili ya uzinduzi wa album yake hapo kesho au iwapo kikao hicho na wanahabri kina lengo lingine.

Kwa sasa, macho yote yako kwake Alikiba huku mashabiki wakisubiri siku ambayo atadondosha album hiyo.

Leave your comment