Zuchu Aweka Rekodi Mpya YouTube Tanzania

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya Wasafi Zuchu ameendelea kuandika historia kwenye muziki wa Tanzania kwani kwa sasa ndiye mwanamuziki wa kike kutokea nchini Tanzania anayeongoza kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Zuchu Azungumzia Uhusiano wake wa Karibu na Maproducer S2kizzy na Ayo Lizer

Kwa sasa, Zuchu ameshatazamwa takriban mara Milioni 230 kwenye mtandao wa YouTube akifuatiwa na Nandy ambaye ameshatazamwa mara Milioni 125 kwenye mtandao huo mkubwa duniani.

Rekodi hii ya Zuchu inaashiri kuwa ngoma za Zuchu zinakubalika sana na mashabiki kwani kando na kuwa mwanamuziki wa kike kutokea Tanzania aliyetazamwa zaidi YouTube, ilipofika Machi mwaka huu, Zuchu aliweka historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kutokea Tanzania kuwa na wafuatiliaji Milioni moja kwenye mtandao huo.

Ukiweka kando ubora usiomithilika wa ngoma za Zuchu ambazo hufanya mashabiki kusikiliza zaidi ngoma zake, pia Zuchu anafanya vizuri kwenye mtandao huo kutokana na mikakati madhubuti ya lebo yake ya WCB ambayo ina ushawishi mkubwa hapa Afrika Mashariki.

Soma Pia: Nyimbo Kali Zilizowahi Kutoka Mwezi Septemba [Video]

Kwa mwaka huu, Zuchu ameachia ngoma tatu ikiwemo ‘Sukari’ ambayo imeweka rekodi ya kuwa wimbo ambao umetazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa mwaka huu wa 20121 barani Afrika.

Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 53 kwenye mtandao wa YouTube. Kwa sasa Zuchu anatamba na ngoma ya ‘Yalaaaa’ ambayo imetoka wiki nne zilizopita.

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Leave your comment