Zuchu Azungumzia Uhusiano wake wa Karibu na Maproducer S2kizzy na Ayo Lizer

[Picha: Capital News]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki Zuchu ameelezea uhusiano wa karibu aliyonao na watayarishaji wa muziki kutoka lebo ya WCB. WCB kama vile lebo nyingi iko na watayarishaji wake wa muziki ambao wanachangia pakubwa katika mafanikio ya nyimbo za wasanii waliopo kwenye lebo hiyo.

Soma Pia: Zuchu Ajibu Madai ya Kutumia Ushirikina Ili Kupata Mafanikio Kwenye Muziki

Watayarishaji wao wa muziki ni pamoja na S2kizzy na Ayo Lizer. Zuchu akiwa mmoja wa wasanii waliosainiwa chini ya WCB ameweza kufanya kazi na Ayo Lizer na S2kizzy.

Katika mahojiano ya hivi karibuni, Zuchu aliulizwa kuchagua mmoja katika ya hao wawili ambaye yeye kama msanii anamkubali sana. Zuchu hata hivyo alishindwa kwani amekuwa na ukaribu mno na S2kizzy na Ayo Lizer na hata kufanya kazi nao katika mandhari tofauti.

Soma Pia: Zuchu Amsifia Nandy, Adokeza Kuwa Hana Tatizo Kufanya Kolabo Naye

Msanii huyo alieleza kuwa amepata fursa ya kufanya kazi na Alizer katika hali ngumu. Alifichua kuwa kuna muda Ayo Lizer alishughulikia wimbo wake japo alikuwa anaugua ugonjwa wa Korona.

Zuchu vile vile aliongeza kuwa ngoma zote kutoka lebo ya WCB hupitia mikononi mwa Ayo Lizer. Kwa upande mwingine, S2kizzy ndiye amesimamia ngoma nyingi za Zuchu. Alisema kuwa licha ya ukaribu wake na Ayo Lizer, amefanya ngoma nyingi sana na S2kizzy na hivyo basi amechangia pakubwa katika safari yake ya muziki.

Lizer na S2kizzy ni miongoni mwa watayarishaji wa miziki wanoheshimika katika tasnia ya burudani ya Tanzania.

Japo wawili hao wanafanya kazi katika lebo moja, hapo awali tetesi ziliibuka mtandaoni zikiashiria kuwa huenda hawako katika hali ya mazungumzo.

Leave your comment