Otuck Azungumzia Ukosefu wa Amapiano Kwenye EP Yake Mpya ‘Future Memories’

[Picha: Otuck Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipuizi Otuck kutokea lebo ya Makini Records amefunguka kuhusu kukosekana kwa mtindo wa Amapiano kwenye EP yake mpya iliyopewa jina la 'Future Memories'. Otuck amekuwa gumzo mitandaoni kutokona na mapokezi mazuri ambayo EP yake ilipata.

Soma Pia: Maua Sama Afunguka Kuhusu Tatizo la Kiafya Lilioathiri Utendakazi Wake Kimuziki

Uzinduzi wa EP hiyo ulihudhuriwa na mastaa wakubwa nchini Tanzania na hivyo basi kuifanya nyota ya Otuck Kung'aa hata zaidi kimuziki. Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Otuck alieleza sababu kuu ya mtindo wa Swahili Amapiano ambao unavuma sana kwa sasa, kukosekana kwenye EP hiyo ambayo iko na ngoma tano.

Otuck alisema sababu kuu ni kuwa wakati akirekodi nyimbo zilizoko kwenye EP, mtindo wa Swahili Amapiano ulikuwa bado haujatambulika. Aliongeza kuwa yeye pia alitaka kuimba nyimbo ambazo zitadumu hadi siku za usoni, na wala si nyimbo ambazo zitaisha wakati upepo wa Swahili Amapiano utatulia.

Soma Pia: Zuchu Ajibu Madai ya Kutumia Ushirikina Ili Kupata Mafanikio Kwenye Muziki

Kulingana na Otuck, jina alilolipa EP yake ambalo ni 'Future Memories', au ukipenda kumbukumbu za usoni katika lugha ya Kiswahili, ndilo lililomuelekeza katika ngoma alizofanya.

"Nyimbo nyingi kwenye EP nilizirekodi wakati Amapiano bado haijaanza kulia. Honestly izi nyimbo zote wakati nazirekodi Amapiano ilikuwa ni bado na of course ni nyimbo nzito, nyimbo kubwa na mimi sio msanii ambaye nisema nataka kufuata trends, mimi I want to set my own trend. Ndio maana ata hii EP ikaitwa future memories, ina maana huu ndio muziki ambao tutakuja kusikiza baadae," Otuck alisema.

Leave your comment