Nyimbo Mpya: Meja Kunta Aachia Wimbo Mpya ‘Simba’

[Picha: Meja Kunta Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bingwa wa muziki wa Singeli nchini Tanzania Meja Kunta ameamua kukosha hisia za mashabiki wa mpira wa miguu baada ya kuachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Simba’.

Meja Kunta ambaye hujitanabaisha na kujinadi kuwa mshabiki wa nguli wa klabu ya Simba ametoa ngoma hii ikiwa ni siku chache zimebaki kufikia kilele cha tamasha la Simba Day ambalo hurindima kila mwaka.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya za Singeli Zinazofanya Vizuri Bongo

Kwenye wimbo huu Meja Kunta anaonesha namna Klabu ya Simba ina uwezo mkubwa ukilinganisha na timu pinzani ambazo huchuana na Simba.

Kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu Meja Kunta anaimba: "Simba kimataifa taifa wapinzani mtasubiri washindi wa vikombe na medali mpira biriani kachumbari muulize Mama J anajua.”

Ngoma ya ‘Simba’ ni kazi nzuri ya mtayarishaji wa muziki Eyo Kenny ambaye anasifika kwa kutengeneza nyimbo za singeli na ambaye ameshafanya kazi na wasanii wengi wa singeli kama vile Balaa Mc pamoja na Dulla Makabila.

Soma Pia: Meja Kunta Aitaja Singeli Kuwa Muziki Bora Zaidi Tanzania

Kwa miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwa na utaratibu wa wanamuziki kuachia nyimbo ambazo zinasifia klabu zao kwani wiki chache nyuma Nandy alitoa wimbo wake wa 'Yanga' huku wasanii kama Diamond Platnumz,Tundaman pamoja na Whozu ambazo wameimbia klabu ya Simba.

Kabla ya kibao hiki Meja Kunta alikuwa anatamba na wimbo wake unaoitwa ‘Kidimbwi’ ambao ulitoka miezi mitatu nyuma na ni ngoma ambayo imefanya vizuri sana hapa nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=0JNrI7WMXbM

Leave your comment