Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya za Singeli Zinazofanya Vizuri Bongo
14 July 2021
[Picha: YouTube]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Ikiwa inatimia takribani mwezi mmoja tangu Zuchu aachie wimbo wake wa ‘Nyumba Ndogo’ ambao umefanya vizuri sana, wasanii wengine pia kutokea nchini Tanzania wameamua kutoa nyimbo zao za Singeli.
Soma Pia: Wasanii 5 Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Kwenye YouTube Tanzania
Kando na Nyumba Ndogo, zifuatazo ni nyimbo tano za Singeli zinazofanya vizuri nchini Tanzania:
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano za Zuchu, Diamond, Alikiba na Rayvanny Zinazovuma YouTube
Demu wangu - Bright ft Meja Kunta
Julai 17 msanii Bright alishangaza mashabiki baada ya kuachia video ya wimbo wake ‘Demu Wangu’ akiwa ameshirikiana na Meja Kunta. Wimbo huu unakuja miezi kadhaa baada ya Bright kuchukua likizo ya kufanya muziki na mapokezi ya wimbo huu yamekuwa ni makubwa yakichagizwa hasa na ubora wa video hiyo ambayo imeongozwa na Jay huku audio ikitayarishwa na Kenny na kufikia sasa wimbo huu umeshatazamwa takribani mara laki moja na kumi elfu.
Ex Wangu Remix - Hamisa Mobetto
Kutokea Mobetto Music, Hamisa Mobetto Julai 9 aliachia remix ya Ex wangu akiwa na Seneta Kilata. Hamisa aliweka wazi kuwa kufanya Singeli kuna utofauti na kufanya aina nyingine ya muziki lakini aliamua kuimba Singeli kwani ni muziki wa halisi kutoka Tanzania.
Stress - Balaa MC
Baada ya kutamba na wimbo wake wa ‘Nakuja’ Balaa Mc ameamua kurudi na singeli safi inayoitwa ‘Stress’. Kwenye wimbo huu uliotoka June 24, Balaa MC anaeleza jinsi changamoto za kila siku kama mapenzi na kulipa kodi zinampa mawazo. Kufikia sasa, video ya wimbo huu iliyoongozwa na Black X ishatazamwa takriban mara laki mbili kwenye mtandao wa YouTube.
Nyumba Kubwa - Meninah
Tangu aanze muziki mwaka 2012 Meninah hakuwahi kufanya Singeli ila June 24 mwaka huu, aliona ndio muda muafaka wa kufanya hivyo na tangu atoe ‘Nyumba Kubwa’, mashabiki na pasi na shaka watu wengi wameonekana kupendezwa na wimbo huo.
Ndio Basi Tena - Manfongo ft Stamina
Baada ya ukimya wa muda mrefu Julai 3 mwaka huu , Manfongo amerudi na "Ndio basi tena" akimshirikisha Stamina. Wimbo huo unapatikana kwenye EP yake ambayo aliitoa hivi karibuni.
Leave your comment