Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia ‘Essence’ Remix

[Picha: Muziki Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea Kings Music Tommy Flavour ameachia remix ya wimbo ‘Essence’ wa Wizkid aliomshirikisha Tems unaofanya vizuri duniani.

Tommy Flavour kupitia akaunti yake ya Instagram amechapisha video fupi inayomuonesha akiwa yuko baharini huku akitumia mdundo wa ‘Essence’  kuweka mashairi yake ambayo bila shaka yamekosha sana mashabiki.

Soma Pia: Quick Rocka Aeleza Sababu ya Kutomshirikisha Msanii Yeyote Kwenye EP Yake

"Ulisema kuenda huwezi huko nje ni ngumu manage penye miti hamna wajenzi. Unaogopa kuteswa na wezi kuumizwa," anaimba Tommy kwenye remix hiyo.

Mara ya mwisho kwa msanii Tommy Flavour kusikika ilikuwa ni kwenye ‘Ndombolo’ wimbo ambao ulitoka Juni mwaka huu akiwa ameshirikiana na Alikiba, K2ga pamoja na Abdu Kiba.

Tommy ni msanii wa tatu kutokea Tanzania kufanya remix ya wimbo wa ‘Essence’ kwani rapa kutokea Intersource records Young Lunya alifanya ‘Essence Freestyle’ siku moja iliyopita na Country Wizzy pia kutokea Konde Gang alifanya freestyle ya wimbo huo siku chache nyuma.

Soma Pia: Diamond Aeleza Sababu ya kuachia Wimbo Wake Mpya 'Naanzaje'

‘Essence’ ni wimbo wa Wizkid ambao umepata mafanikio makubwa sana tangu kuachiwa kwake kwani wimbo huo umeweza kupenya mpaka kwenye chati za Billboard za Marekani na kuingia kwenye orodha ya nyimbo 20 bora nchini humo.

Kando na mastaa wa kitanzania ambao wameonekana kufanya remix ya wimbo huo pia Da Baby kutokea nchini Marekani siku chache nyuma alifanya ‘Essence Freestyle’.  Justin Bieber pia alivutiwa na wimbo huo na hivyo kuachia ‘Essence Remix’ wiki kadhaa nyuma.

Tazama Video ya Tommy Flavour HAPA.

Leave your comment