Diamond Aeleza Sababu ya kuachia Wimbo Wake Mpya 'Naanzaje'

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Diamond aliachia video rasmi ya wimbo wake mpya wa 'Naanzaje' mnamo tarehe tano mwezi huu. Video hiyo ilipokelewa vizuri na mashabiki na kutazamwa zaidi ya mara milioni moja chini ya siku moja.

Diamond amejitokeza na kutoa maelezo kuhusu ngoma hiyo ambayo kwa sasa inavuma sana mtandaoni. Kwa mujibu wa taarifa aliyoichapisha mtandaoni, Diamond alidai kuwa hakuipa fikra sana ngoma hiyo na nia yake halisi ilikuwa kuwapa mashabiki wake zawadi.

Soma Pia: Zuchu Achochewa Kuongeza Bidii Baada Ya Tems Kushirikishwa Kwenye Albamu Ya Drake

Ila baada ya ngoma hiyo kutoka ilipendwa sana na wengi na kumfanya kupata mtazamo tofauti kuihusu. Alieleza kuwa kadri muda unavyosonga ndivyo yeye mwenyewe pia anapata mtazamo tofauti kuhusu ngoma hiyo na kuipenda zaidi.

Aidha, Diamond alisimulia jinsi wimbo huo unamkumbusha mapenzi yake ya kale. Alisema kuwa anakumbuka maisha na mpenzi wake wa zamani ambako walikuwa wanapendana sana na maisha yalikuwa matamu siku hizo.

"Nikiitazama hii video, hususan kipande hiki nakumbuka mbali sana...enzi za Mahaba mazito na Madam....Enzi ambazo tulikuwa tunajifungia chumbani wiki nzima, nakwepa kurecord na ata show ikitokea naitaftia sababu ya kutokuwepo....kiukweli wimbo huu wakati nautoa, sikuuchukulia serious....niliutoa tu kama bonus kwakujua mashabiki zangu wamenimiss kunisikia nikiimba hivyo..Licha ya kupokelewa na Kupendwa sana ulivyotoka...for some reason kadri muda uendanvyo nimejikuta naupenda saana, na mbaya zaidi kila niusikiapo unanifanya nitamani tena kumpenda mtu, na kuwa tena wenye Mahusiano......japo ghafla akili timamu hunijiaga, na kunambia "Simba Jifocusie zako kwenye kazi mwaya," Diamond aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Soma Pia: Nyimbo Tano Zinazotamba YouTube Tanzania wiki hii

Wakati wimbo wake wa 'Naanzaje' unavuma katika anga za burudani, mashabiki bado wanasubiri Diamond kudondosha albamu yake. Albamu ya Diamond intarajaiwa kutikisa anga za muziki kwani utayarishaji wake umewahusisha wadau waliotajika ulimwengu mzima.

Leave your comment