Quick Rocka Aeleza Sababu ya Kutomshirikisha Msanii Yeyote Kwenye EP Yake

[Picha: Quick Rocka Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Quick Rocka ameweka wazi sababu ya kufanya EP yake ya ‘Love Life’ pekee yake bila kumshirikisha msanii yeyote yule.

Quick Rocka ambaye ni mojawapo kati ya marapa bora sana nchini Tanzania aliachia EP yake ya ‘Love Life’ Agosti 5 mwaka huu ikiwa imesheheni nyimbo nne ambazo ni ‘Love Song’, ‘Teamo’, ‘Ukimya’, pamoja na ‘Kabinti’ na kati ya hizo hakushirikisha mwanamuziki yeyote.

Soma Pia: Nyimbo Tano Mpya Tanzania Wiki Hii Kutoka kwa Benpol, Killy,Rich Mavoko na Nay wa Mitego

Akizungumza kwenye kituo cha Times Fm, Quick Rocka ameeleza kuwa hakuona umuhimu wa kushirikisha msanii yeyote kwenye mradi huo kwani kabla ya EP hiyo, alikuwa ameshafanya kazi na wasanii wengi hivyo akaona abadilishe nia kwa kufanya EP hiyo mwenyewe.

"Nyimbo za nyuma kabla ya kuachia hii EP nyingi zinakuwa nikishirikiana na na watu kwa hiyo nikaamua iwe tofauti na hata jina ni Love Life inaelezea maisha ya kimapenzi hivyo nikaamua iwe iwe ya tofauti. Kwa hiyo its me naongea na watu in a love language," alizungumza msanii huyo.

Soma Pia: Hanscana Ajibu Madai Kuwa ‘Naanzaje’ ya Diamond Inafanana na ‘Fever’ ya Wizkid 

Ukweli ni kwamba pamoja na EP kutoshirikisha msanii yeyote, kazi hio bado imenoga sana kwani Quick Rocka ameweza kuitendea haki .

Aidha, kwenye mahojiano hayo, Quick Rocka amesema kuwa baada ya ‘Love Life’ atarejea kufanya kazi na wasanii wengine kama ilivyo kawaida yake.

"Baada ya EP hii nyimbo nyingine zitakuwa ni collabo na watu tofauti tofauti," alidokeza Quick Rocka.

Leave your comment