Nyimbo Tano Mpya Tanzania Wiki Hii Kutoka kwa Benpol, Killy,Rich Mavoko na Nay wa Mitego

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Unapenda muziki mzuri? Basi bila shaka makala hii ni kwa ajili yako kwani tumezikusanya nyimbo mpya kali tano zilizotoka wiki iliyopita kutoka kwa wasanii nchini Tanzania:

Soma Pia: Nyimbo Tano Zinazotamba YouTube Tanzania wiki hii

Ndo Maana - Rich Mavoko

Kwenye ‘Ndo Maana’, Rich Mavoko anaonesha namna ambavyo mapenzi yanamuumiza kutokana na kuachwa na mpenzi wake aliyemuamini na kumpenda. Abydady ndiye amehusika kutayarisha wimbo huu. Kando na wimbo huu, amehusika kuandaa nyimbo kama ‘Iyena’ ya Diamond Platnumz pamoja na ‘Aje’ ya AliKiba.

https://www.youtube.com/watch?v=iitIRSfllj0

Ni Wewe - Killy ft Harmonize

Killy anaendelea kupeperusha vyema bendera ya Konde Gang baada ya kuachia ngoma yake ya ‘Ni wewe’ aliomshirikisha mwalimu wa Amapiano Harmonize. ‘Ni wewe’ umekopa baadhi ya vionjo kutoka kwenye wimbo wa Les Wanyika uitwao ‘Sina Makosa’. Ubunifu huo kutoka mtayarishaji Hunter ndio umefanya wimbo huu kukubalika sana na mashabiki kwani kufika sasa wimbo hushasikilizwa takribani mara Laki nne sitini na nane kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ixzllSyWSdU

Bia - Benpol

Benpol anaonekana kutoka nje ya Boksi kwenye wimbo wake mpya wa ‘Bia’ kwani ametumia mahadhi ya Amapiano kwa mara ya kwanza tangu aanze muziki. Kama jina linavyojieleza ‘Bia’ ni wimbo ambao unaongelea pombe na jinsi inavyowakosha watumiaji wake.

https://www.youtube.com/watch?v=GWCMby_71pk

Rais wa Kitaa - Nay Wa Mitego

Nay wa Mitego ni zaidi ya kipaza sauti kwa watanzania na hilo limedhihirishwa kwenye wimbo wake mpya wa ‘Rais wa Kitaa’ ambao amegusia maeneno nyeti kama tozo za simu, hali ya kisiasa nchini Tanzania na mengineyo mengi. Kufikia sasa, wimbo huu umetazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=0AEyaLhZR8E

Simba Ni Noma - Whozu ft Donat Mwanza

Mwanamuziki Whozu ameamua kuanika dhahiri shahiri mapenzi aliyonayo kwa timu yake ya Simba kupitia wimbo wake mpya wa "Simba Ni Noma" aliomshirikisha Donat Mwanza. Mashairi ya wimbo huu yanasifia ubora wa timu ya Simba na kuonesha ni kwa namna gani Simba ina viwango vya juu kwenye soka la nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=545eCLT9fdY

Leave your comment