Nyimbo Mpya: Ben Pol Aachia Wimbo wa ‘Bia’

[Picha: Ben Pol Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bingwa wa muziki kutokea nchini Tanzania Ben Pol ameaachia wimbo mpya kwa jina ‘Bia’ akimshirikisha Jaco Beats.

Ben Pol ambaye hufahamika sana kwa nyimbo zake nzuri zenye vionjo vya RnB kwenye kibao hiki amechukua sura mpya kwa kutembea kwenye mdundo wa Amapiano ambao ni maarufu sana Tanzania kwa sasa.

Soma Pia: Ben Pol Aeleza Jinsi Upungufu wa Tuzo Umeathiri Tasnia ya Muziki Tanzania

‘Bia’ kama jina linavyosadifu ni wimbo unaoongelea kuhusu pombe na jinsi ambavyo inawafurahisha na kukosha watumiaje wake.

Ukimjulisha na mdundo wenye nguvu unaonogesha wimbo huu, basi bila hiyana kibao hiki kitatamba sana kwenye clubs mbalimbali hapa Tanzania.

Kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu, mtunzi anabainisha sifa za ‘Bia’ kwa kuimba "Usifananishe na kitu chochote (bia), ebu ipe heshima bwana (bia), mhudumu we fanya unipe (bia) mie nipe kichwa kichangamke."

Soma Pia: Ben Pol Asimulia Masaibu Aliyopitia Kwenye Tamasha lake la Kwanza Kabisa

Wimbo huu umetayarishwa na Daxo Chali na bila shaka ameweza kuonesha ufundi mkubwa sana kwani ametengeneza mdundo wenye nguvu na unaovutia sana.

Aidha, Daxo ni mojawapo ya watayarishaji muziki bora sana nchini Tanzania ambaye ameshafanya kazi na wasanii kama Dogo Janja, Country Boy na Young Lunya.

Wimbo huu unamuongeza Ben Pol kwenye orodha ya wasanii wa Tanzania ambao wameshafanya muziki wa Amapiano wengineo ni kama Harmonize, Baba Levo, Damian Sol, Ommy Dimpoz, Rayvanny, Aslay pamoja na Diamond Platnumz.

https://www.youtube.com/watch?v=GWCMby_71pk

Leave your comment

Top stories

More News