Ben Pol Aeleza Jinsi Upungufu wa Tuzo Umeathiri Tasnia ya Muziki Tanzania

[Picha: Ben Pol Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Upungufu wa tuzo umeathiri pakubwa utendakazi wa wasanii na ubora wa nyimbo katika tasnia ya muziki ya Tanzania; hii ndio kauli ya mwanamuziki Ben Pol ambaye alifunguka katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni.

Ben Pol anaamini kuwa tuzo zilichangia pakubwa katika kujenga tasnia ya muziki na kwa kiasi kikubwa kukuza ubora wa nyimbo.

Soma Pia: Ben Pol Asimulia Masaibu Aliyopitia Kwenye Tamasha lake la Kwanza Kabisa

Ben Pol ambaye ni mmoja wa wasanii ambo wamekuwepo kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu sana, alisema kuwa hapo awali tuzo ndio ilikuwa kigezo cha kuorodhesha wasanii na kupima uwezo na ubora wao.

Hata hivyo, ukosefu wa tuzo umeleta vigezo vingi sana vya kulinganisha wasanii na hivyo basi ni ngumu kuwaeka wasanii katika mizani moja. Ben Pol alitoa mfano kuwa, tuzo ziliweza kuwakea wasanii wote kwa mizani moja na kupima utunzi, ushairi naubunifu wao katika kutengeneza nyimbo bora.

Aliongeza kuwa kwa sasa, wasanii wanapigania na kujipima kwa kutumia vigezo kama vile umaarufu, kuvuma mtandoni na masuala mengine ambayo kwa kiasi fulani hayachangii katika ubora wa muziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Benpol Aachia EP Mpya ‘B’

Msanii huyo alieleza kuwa ni vigumu sana msanii chipukizi kutambuliwa katika tasnia ya muziki ya leo kwa sababu ya mkanganyo uliopo na ubishani wa wasanii tajika.

"Zamani tuzo zilikuwa zinatueka mzani mmoja; mwenye mtaji mkubwa kwa muziki, mwenye mtaji mdogo na mwenye mtaji wa katikati. Kinachoangaliwa ni uwezo, uandishi, uimbaji mzuri, ufundi wa kupanga mashairi, ustadi wa kupanga muziki.

“Tulikuwa tumeekwa kwenye mzani huo mmoja. Lakini sasa hivi, mizani imekuwa mingi, kuna mzani wa views, kuna mzani wa kujaza show, yaani mizani imekuwa mingi mingi. Mzani wa kuonekana sana, nani anaonekana sana kuliko mwingine, nani anapiga interview nyingi, nani anatrendi, kwa hiyo mizani imekuwa mingi. Wakati zamani kulikuwa na mzani mmmoja tu wa ubora wa kazi," Ben Pol alisema.

Leave your comment