Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video ya ‘Yanga’ Akisifia Timu ya Yanga FC

[Picha: Capital FM]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka Tanzania Nandy ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Yanga’, akiisifia timu ya kandanda ya Yanga FC.

Ngoma hiyo inasifia ubabe wa timu ya Yanga katika kutinga magoli. Nandy pamoja na wanadensi wake wanaonekana wakiwa wamevaa sare za Yanga huku wakiwa katika uwanja wa Kandanda.

Soma Pia: Nandy Atangaza Tarehe Rasmi Atakayopeleka Nandy Festival Dar es Salaam

Nandy pia kupitia ngoma yake alimkaribisha mkufunzi mpya wa Yanga Haji Manara. Haji Manara hapo awali alikuwa akifanya kazi na timu ya Simba kabla ya yeye kuondoka na baadaye kujiunga na Yanga.

"Wewe Manara karibu nyumbani baba hakatai mtoto wewee," Nandy aliimba.

Kuondoka kwa Manara kutoka timu ya Simba kulimfanya mwanamuziki nyota kutokea lebo ya WCB Diamond Platnumz kuchapisha ujumbe mtandaoni akikiri kuwa alikuwa ameachwa na maumivu.

Diamond ambaye ni shabiki sugu wa timu ya Simba alimsifia Manara. Aidha, upekuzi wa mwandishi huu umebaini kuwa chapisho hilo la Diamond halipo tena katika ukurasa wake wa Instagram.

Soma Pia: Nandy: Ilinigharimu Milioni 40 Kufanya Wimbo wa ‘Leo Leo na Koffi Olomide

Aidha, Diamond pia mwaka jana aliachia ngoma ya kuisifia timu ya Simba. Ngoma hiyo ambayo ilichapishwa katika akaunti yake ya YouTube kufikia sasa imetazamwa takriban mara milioni mbili.

Kwa sasa ngoma hiyo imezidisha upinzani baina ya timu hizo mbili huku kila shabiki akivuta kamba upande wake na kuisifia timu yake.

https://www.youtube.com/watch?v=Zq4y7S6DfL8

Leave your comment